Fahari ya Serengeti

Friday, March 31, 2017

JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA


Serengeti Media Centre.

Joseph Nyiboha(22)mkazi wa kijiji cha Borenga wilayani Serengeti Mkoani Mara amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela  kwa kosa la kubaka na kumpa mimba mwanafunzi aliyekuwa amechaguliwa na kujiunga na  kidato cha kwanza Machochwe sekondari.
Hata hivyo  mshitakiwa wakuwepo mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa alitoroka baada ya kudhaminiwa.
Kabla ya kutolewa adhabu hiyo mwendesha mashitaka wa Jamhuri Jakobo Sanga Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile  akisoma maelezo katika kesi ya jinai namba 87/2016 ,alisema mshitakiwa alifikishwa mahakamani akikabiliwa na makosa matatu ya jinai.
Alitaja kosa  la kwanza kuwa ni kuishi na mwanafunzi kinyume na kifungu 134 cha Sheria ya Elimu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, na kosa la pili ni kumbaka mwanafunzi wa miaka 15 aliyetarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza Machochwe sekondari 2016 ikiwa ni kinyume na kifungu namba 130(1)na(2)(e)na namba 131(1)cha sheria ya ubakaji sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Sanga aliiambia Mahakama kuwa kosa la tatu ni  kumpa mimba mwanafunzi kinyume na kifungu namba 35(3)na(4)sheria ya Elimu sura ya 353 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mshitakiwa alikamatwa Oktoba 24 mwaka 2015 nyumbani kwake katika kijiji cha Borenga  baada ya kubainika kuishi na Mwanafunzi wa shule ya msingi Borenga aliyekuwa amechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  Machochwe,hata hivyo alikuwa tayari ni mjamzito,na kuomba adhabu kali itolewe.
 Hakimu Ngaile alisema ushahidi  uliotolewa mahakamani haukuacha shaka”mahakama yangu inatoa adhabu kali kwa mshitakiwa ,katika kosa la kwanza atatumikia  kifungo cha miaka 5 jela, kosa la pili   kifungo cha miaka 30  jela na kosa la tatu atakwenda jela miaka 30 adhabu zote zitakwenda pamoja atatumikia miaka 30”alisema.
mwisho.

0 comments:

Post a Comment