Fahari ya Serengeti

Saturday, September 30, 2017

KIKAO CHA WAZEE WA MILA MUUNGANO INCHUGU CHATOA TAMKO ZITO


 Wazee wa mila wa koo ya Inchugu Muungano wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakiwa nje ya Mstu mkubwa ambao wanadai ni ikulu yao katika kijiji cha Nyamakendo mara baada ya kikao chao ambapo wametoa azimio la kuwa koo hiyo haitajihusisha na ukeketaji na watakao kaidi watawashughulikia.




 Wazee wa mila wakiwa wanatawanyika
 Baada ya kikao wanakaa pamoja kwa kula na kunywa huku wakijadili mambo yanayohusu mila na desturi zao






 Kabla ya chakula unaanza na togwa

MRADI WA TOKOMEZA UKEKETAJI SERENGETI WAWAKUMBUKA WAHUDUMU WA AFYA VIJIJINI

 Meneja wa Maradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti Godfrey Matumu kulia akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu msaada wa baiskeli na vifaa vingine vya kazi kama mabegi,tisheti na kofia  ukiwa na thamani ya sh 34 mil,kwa ufadhili wa UN WOMEN ,kwa ajili ya Wahudumu wa Afya vijijini ambao wanaelimisha jamii mambo mbalimbali ya afya ikiwemo kupiga vita vitendo vya ukeketaji.
Mradi huo unatekelezwa na shirika la amref health africa,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)Halmashauri na wadau wengine.

 Dc Nurdin Babu kushoto akimkabidhi Mhudumu wa Afya Vijijini Julius Antony Baiskeli na vifaa vingine kwa ajili ya kuendeleza kazi za utoaji elimu na kupinga ukeketaji wa watoto wa kike.
 Nakukabidhi baiskeli uitumie kwa kazi kusudiwa isiwe ya kusombea mkaa na vimoro,dc anasisitiza.
 Dc anamkabidhi kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Serengeti Deo Kisaka vifaa hivyo ili aweze kuwapa wahudumu wa afya vijijini.

 Kila mmoja na mchuma wake kwa ajili ya kuingia kazini
 Picha ya Pamoja ilipigwa








 Katibu Tawala wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara akisisitiza uwajibikaji wa wahudumu wa afya vijijini

 "Nendeni mkasaidie jamii hasa wajawazito na watoto wakike wasikeketwe,"anasema Dc





Thursday, September 28, 2017

JELA MIAKA 10 KWA KUKUTWA NA VIPANDE 7 VYA NYAMA YA NYUMBU

Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara imewahukumu washitakiwa wawili kwenda jela miaka 10 ama kulipa faini ya sh 5mil kwa kukutwa na vipande saba vikavu vya nyumbu vyenye thamani ya sh 1.4 mil.

Akitoa hukumu Hakimu Amalia Mushi amesema washitakiwa Magasi Metache Nyantito(31)wa Parknyigoti na Thomas Ng'ora Mrengi(22)mkazi wa kijiji cha Miseke ambaye hakuwepo Mahakamani baada ya kuruka dhamana,amesema washitakiwa wametiwa hatiani kwa makosa matatu waliyoshitakiwa nayo.

Ambayo ni kukutwa ndani ya hifadhi,kukutwa na silaha ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kumiliki nyara za Taifa vipande saba vikavu vya nyumbu kinyume cha Sheria.

Hata hivyo amesema mlango wa rufaa uko wazi kama hawataridhishwa na maamzi hayo na mshitakiwa amepelekwa gerezani.

WAZEE WA MILA WATAKIWA KUTOBADILI MSIMAMO WAO KUHUSU UKEKETAJI

 Wakazi wa kijiji cha Bisarara kata ya Sedeco wilaya ya Serengeti wamewataka wazee wa mila wa koo ya Inchage kutokubadilika na baadae kuruhusu ukeketaji kuendelea katika jamii.
Katika Mkutano wa wahadhara wa wazee wa mila katika kijiji cha Bisarara wamesema kuwa uamzi wa wazee wa mila wa kupiga marufuku ukeketaji unalenga kumkomboa mtoto wa kike ,hivyo wanatakiwa kutoyumba na baadae kuwaruhusu kisirisiri kuendelea na ukeketaji.
 Msanii wa Nuru Sanaa akitoa elimu kwa wakazi wa kijiji cha Bisarara
 Wasanii wakitoa elimu ya aathari ya ukeketaji









ILI KUPANDISHA HADHI ZAHANATI YA BUSAWE,HALMASHAURI YATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA WODI

 Halmashauri ya wilaya ya Serengeti imetakiwa kutoa fedha za ujenzi wa wodi zahanati ya Kisaka na kukamilisha baadhi ya majengo ili kuiwezesha serikali kuipandisha hadhi na kuwa Kituo cha Afya.
Naibu Waziri wa Afya Dk Hamisi Kigwangala amesema kufanya hivyo kutakuwa kumeongeza maeneo maalum ya kutolea huduma za afya kwa wananchi wake.
"Wakazi wa hapa waishio nje wamejitahidi sana kwa ujenzi wa zahanati hii ili kuhakikisha wananchi wa maeneo haya wanapata huduma za afya karibu ,halmashauri kazi iliyoko mbele yenu ni kutoa fedha za kukamilisha baadhi ya miundo mbinu ili iweze kupandishwa hadi,"amesema.
Mapema kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo William Makunja amesema wametenga sh 24 mil kupitia mapato ya ndani ili kusaidia ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali.

 Diwani wa kata ya Busawe Ayobu Makuruma akielezea walivyofanikiwa kujenga zahanati hiyo na mikakati yao ya baadae