Fahari ya Serengeti

Wednesday, May 9, 2018

HOTEL YA FOUR SESSION YAJENGA JIKO LA KISASA LA ZAIDI YA SH 30 NYUMBA SALAMA.



 Hotel ya Four Session imejenga jiko la kisasa la kutumia gesi lenye thamani ya sh 30 mil katika Kituo cha Nyumba Salama Mugumu Serengeti ikiwa ni mwendelezo wa misaada wanayotoa kwenye kituo hicho.

Meneja wa Kitengo cha Utoaji huduma kwa jamii na Ahmed amesema lengo lao ni kuhakikisha uhifadhi wa mazingira unadumishwa kwa kuachana na matumizi ya kuni na mkaa,aidha amesema wanategemea kujenga uzio wa matofali na kuboresha vyoo katika kituo hicho.
 Mtaalam wa Kampuni Chabhoke iliyojenga jiko hilo Sylivester akitoa maelezo jinsi ya matumizi yake.
 Mchungaji na maafisa wa Four Session wakiangalia mradi huo.
 maelezo yanatolewa
 Askofu wa dayosisi ya Mara kanisa la Anglikan Dk George Okoth akiwa na baadhi ya viongozi katika makabidhiano ya jiko hiilo.


 Picha ya pamoja ikapigwa
 Askofu Dk George Okoth ameishukuru kampuni ya Four Session inayoendesha hotel ya kitalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa misaada yake kwa kituo cha Nyumba Salama ambacho kiko chini ya kanisa hilo.
Merina Galibona mratibu wa Kituo hicho akiwaeleza wageni mazingira ya kituo na mahitaji yao

0 comments:

Post a Comment