DED NAOMI NNKO NA DC ALLY MAFUTAH NDIYO WAKISIKILIZA NASAHA TOKA KWA WAHITIMU KABLA YA KUWAKABIDHI ZAWADI.
HERI MTANISA MRATIBU WA MPANGO AKITOA MAELEZO JINSI ULIVYOTEKELEZWA HADI VIJANA 28 WAKAFUZU MAFUNZO YA UFUNDI CHUO CHA CHIPUKA.
DC AKIKABIDHI VIFAA
WAMAZINGIRA MAGUMU WAHITIMU .
Na SERENGETI MEDIA CENTRE
Novemba19,2015.
Zaidi y ash
34 milioni zimetumika kugharamia masomo ya ufundi na kuwanunulia vifaa vya
kazi vijana 28 wanaoishi katika Mazingira magumu wilayani Serengeti Mkoa wa Mara kupitia kitengo
cha Tacaids.
Mratibu wa
Mpango wa kudhibiti Ukimwi halmashauri hiyo Heri Msanisa, amesema hayo wakati
wana wakiwakabidhi vijana hao vifaa
kwenye ukumbi wa halmashauri amesema gharama hizo zilijumuisha ada,chakula na
malazi ,lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kujitegemea.
.
Mkuu wa
wilaya hiyo Ally Mafutah akikabidhi
vifaa kwa vijana hao kutoka kata 28 amesema lengo la serikali kupitia mpango
huo ni kuwawezesha kujiajiri kupitia taaluma hiyo,na kuwasisitiza kuunda
vikundi vya kazi ili waweze kuendelea kusaidiwa kwa karibu.
Felista Maro
mmoja wa wahitimu kutoka kata ya Majimoto amesema utoaji wa masomo hayo bila
ubaguzi wa jinsia na kuwa masomo hayo yamewaweza kupata stadi za maisha na
kuomba serikali ihakikishe inawekeza zaidi kwenye eneo la kuwajengea uwezo wa
ufundi vijana wengi ili kuwawesha kujiajiri
Wanafunzi
hao wamefuzu katika masomo ya kozi mbalimbali ikiwemo ufundi
magari,useremala,ushonaji na ujenzi,baadhi tayari wameishaanza kazi za
kujitolea katika makampuni ya watu binafsi
wilayani hapo.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment