Fahari ya Serengeti

Tuesday, September 19, 2017

MNADA WA MIFUGO WATOA SOMO KWA WAFUGAJI WADAI MIFUGO MINGI SI DILI TENA

 Baadhi ya wafugaji wa jamii ya Maasai wa kijiji cha Ololoswakan Loliondo wakichangishana fedha kwa ajili ya kununua mifugo yao wakati wa mnada wa hadhara ulioendeshwa na kampuni ya udalali ya Ubapa Co.Ltd ya Musoma ikiwa ni utekelezaji wa amri ya Mahakama ya kuuzwa kwa ng'ombe 628 ambao walikamatwa ndani ya Hifadhi ya Senapa na Pori tengefu la Loliondo na wenye mifugo kushindwa kujitokeza.
Hata hivyo ng'ombe 618 imeuzwa kwa zaidi ya sh 34 mil na 12 wakidaiwa kufa kutokana na mrundikano,mnada huo umetoa somo kubwa kwa wafugaji hao baada ya kujikuta wanapambana na wanunuzi kutoka maeneo mengine kununua mifugo yao,huku baadhi wakidai kuwa wingi wa mifugo kwa sasa ni dili kwa kuwa unachangia umaskini kwa familia kutokana na ukosefu wa malisho.
 Kila mmoja na fedha yake aking'ang'ana kunusuru mifugo yake
Add caption

 Wanafuatilia matukio ya kuuzwa kwa mifugo yao.


0 comments:

Post a Comment