Mwenyekiti wa Muungano koo ya Inchage Sungura Mturi akitoa tamko la kupiga marufuku ukeketaji kwa wakazi wa Itununu wilaya ya Serengeti ikiwa ni makubaliano ya wazee wa mila wa koo sita wilayani humo kutokomeza ukeketaji kwa watoto wa kike baada ya kupata elimu sahihi ya madhara ya ukeketaji.
Wazee wa mila ambao ndiyo walikuwa vinara wa kusimamia ukeketaji kwa madai ya kutimiza mila na desturi,sasa ni vinara wa kuelimisha jamii kwa kupitia koo zao ,na kuwa watu watakaokaidi watashughulikiwa kwa misingi ya mila na desturi na sheria kwa kuwa zama zimebadilika.
Makubaliano yao ya kutokomeza Ukeketaji yametiwa saini na wazee wa mila wa koo zote mbele ya Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu ,Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref health africa,Kituo cna Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)Halmashauri na wadau wengine chini ya Ufadhili wa UN WOMEN.
Mwaka jana baadhi ya wazee wa mila na ngariba walinaswa na polisi baada ya kujihusisha na ukeketaji na baadhi wamefungwa na wengine kesi zinaendelea mahakamani .
Wananchi wakifuatilia mkutano wa wazee wa mila
Inspekta wa Polisi Alfred Malimi akitoa msimamo wa serikali kwa watakaokaidi maagizo ya wazee wa mila
Wasanii wa Nuru Sanaa wakitoa elimu kwa wakazi wa kijiji cha Itununu
Elimu kwa njia ya Sanaa
0 comments:
Post a Comment