Fahari ya Serengeti

Tuesday, September 19, 2017

NG'OMBE 618 OLOLOSOKWANI ZAPIGWA MNADA KWA AMRI YA MAHAKAMA

 Jumla ya Ng'ombe 618 za wafugaji wa kijiji cha Ololosokwan Loliondo wamepigwa mnada kwa amri ya mahakama baada ya kukutwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori Tengefu la Loliondo na wenye mifugo kushindwa kujitokeza.
Kampuni ya Udalali ya Ubapa Co.Ltd ya Musoma imeendesha zoezi hilo na kufanikiwa kupata zaidi ya sh 34 mil kutokana na mnada huo wa wazi ambao ulihusisha wanunuzi kutoka mikoa ya Arusha na Mara.
Kutokana na operesheni maalum inayoendelea zaidi ya ng'ombe 1500 wamekamatwa za wafugaji wa vijiji vya Ololoswakan na Harashi na kesi iko mahakamani baada ya wahusika kukamatwa nazo.

 Ng'ombe wakiwa katika uzio Kituo cha Krensi cha askari wa hifadhi ya Senapa kwa ajili ya kuhifadhiwa kabla ya zoezi la uuzaji kufanyika
 Safari ya kwenda eneo la mnada inaanza hivyo



Baadhi ya wafugaji waliojitokeza wakati wa mnada kudai mifugo ni yao,lakini wakati wa kukamatwa walikimbia na kushindwa kujitokeza kulipa faini kwa mjibu wa sheria ya wanyamapori

0 comments:

Post a Comment