Fahari ya Serengeti

Thursday, September 7, 2017

WAZEE WA INCHAGE WAJITOKEZA HADHARANI KUPINGA UKEKETAJI

Mwenyekiti wa Koo ya Inchage Muungano Sungura toka Mbalibali akielezea sababu za wazee wa mila kupiga marufuku ukeketaji wa watoto wa kike katika kijiji cha Kisangura wilaya ya Serengeti,na kuwataka wazazi kusomesha watoto wa kike kwa kuwa mila hiyo ni chanzo cha ndoa za utotoni na kuwakandamiza watoto wa kike.
Amesema kwa makubaliano ya wazee wa mila wa koo sita wilayani hapo walioweka saini mbele ya mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu kupitia Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref healtth africa ,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)halmashauri na wadau wengine kwa ufadhili wa UN WOMEN.
Amesema kutokana na makubaliano hayo kila wazee wa koo wanatakiwa kwenda kuongea na jamii yao kupitia mikutano ya hadhara kwa kuwa wazee wa mila ndiyo wanadaiwa kusimamia zoezi la ukeketaji.

Wakazi wa kijiji cha Kisangura wakiwasikiliza wazee wa mila wa koo ya Inchage wakielezea msimamo wao wa kupinga ukeketaji.
Afisa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti William Mtwazi mwenye karatasi akiongea na wazee wa mila wa kata ya Kisangura kabla ya kuanza mkutano wa hadhara,mwenye shati jekundu ni Meneja wa Mradi huo Godfrey Matumu.
Afisa tarafa ya Ikorongo Paul Shanyangi akitoa msimamo wa serikali kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Nurdina Babu kuhusiana na ukeketaji.

Balozi

0 comments:

Post a Comment