|
Naibu Waziri wa Afya Dk Hamisi Kigwangala ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kuhakikisha wanaweka maji na umeme kwenye jengo la Upasuaji Kituo cha Afya Natta haraka ili liweze kutoa huduma kwa wananchi. Dk Kigwangala ambaye amefanya ziara ya siku moja wilayani hapa amesema vyumba hivyo ni muhimu kuwa na maji na umeme ili viweze kutoa huduma kwa wananchi katika mazingira mazuri. Amewataka waganga na wauguzi pia kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya kazi na hilo ndilo kusudi la serikali kwa watu wake. |
Ukaguzi jengo la upasuaji
Dk Kigwangala akipata maelezo toka kwa kaimu mganga mkuu wa wilaya Deo Kisaka
Msisitizo
0 comments:
Post a Comment