Fahari ya Serengeti

Monday, September 4, 2017

KIKUNDI CHA NURU SANAA CHATOA ELIMU YA UNYAGO BILA UKEKETAJI

Wasanii wa Nuru sanaa kutoka Mugumu wilaya ya Serengeti wakitoa elimu ya Unyago bila Ukeketaji katika kijiji cha Kebanchabancha kwa kushirikiana na Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti,wamewakuna wazee wa mila na wananchi ambapo bila ajizi wametoa tamko la kukomesha ukeketaji huku wakiwaambia wafanye unyago bila ukeketaji,tamko hilo la wazee wa mila wa koo ya Inchugu limkoleza elimu iliyotolewa na wasanii hao baada ya kuonyesha faida za Unyago bila ukeketaji na madhara ya ukeketaji.
 Wasanii wakitoa elimu kwa njia ya sanaa,ama hakika zama zimebadilika ,wazee wa mila na wananchi wamesema ukeketaji si dili ,mpango mzima kwa sasa ni Unyago bila ukeketaji.

Kila jambo na watu wake ,hakika wasanii wa Nuru Sanaa Serengeti ni zaidi ya wasanii kutokana na kuvaa uhusika na kufikisha ujumbe kwa jamii.

0 comments:

Post a Comment