Fahari ya Serengeti

Sunday, September 24, 2017

MATARE SERENGETI WAPAZA SAUTI KUPINGA UKEKETAJI

 Wasanii wa Nuru Sanaa wakiwasilisha ujumbe wa athari za ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike hususan ukeketaji kwa wakazi wa Matare Serengeti ambao kwa kuungana na wazee wa mila wamesema ukeketaji hauna nafasi kwa kuwa hauna faida zaidi ya madhara.
Na kuahidi kuongeza kasi kuwasomesha watoto wa kike,kwa kuwa walikuwa gizani sasa nuru Imewawakia na kuomba Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref health africa,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)Halmashauri na wadau wengine kwa ufadhili wa UN WOMEN kuendelea kusambaza ujumbe huo wa mabadiliko kwa jamii kwa kuwa SERENGETI BILA UKEKETAJI INAWEZEKANA.
 Wananchi wanafuatilia igizo
 wako makini kufuatilia ujumbe kupitia igizo
 Wazee wa mila na baadhi ya viongozi wakiwa wanafuatilia mafundisho kwa njia ya sanaa
 Wasanii kazini
 Sanaa hupeleka ujumbe kwa wepesi kwa jamii
 Afisa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti William Mtwazi akisisitiza wananchi kuheshimu kauli ya wazee wa mila waliokataa ukeketaji



0 comments:

Post a Comment