Wasanii wa kikundi cha Nuru Sanaa Serengeti wakiwasilisha elimu kwa njia ya maigizo kwa wakazi wa kijiji cha Mosongo wilaya ya Serengeti juu ya Jando bila ukeketaji katika Mkutano wa hadhara ulioandaliwa na wazee wa mila wa koo ya Inchage ambao wamesema waziwazi kuwa zama zimebadilika ,ukeketaji kwa watoto wa kike ni marufuku,na kuwa jamii ijikite kuwasomesha watoto wa kike.
Wanamwaga sera
Kwa upande wa Burudani hawako nyuma,kwa watu wenye shughuli mbalimbali wasisite kuwasiliana na kikundi hicho.
Igizo la Jando bila Ukeketaji limeibua hisia kwa akina mama na wasichana huku baadhi wakijuta kuwakeketa watoto wao kwa misingi ya kutimiza mila.
Wako kikazi zaidi
Kila mmoja anawajibika kuhakikisha anafikisha elimu sahihi,hakina sanaa inawenyewe
Hawako nyuma pia wanagawa vipeperushi vya madhara ya ukeketaji kwa wananchi ili waweze kupata uelewa,hapo ni jaza ujazwe
Wakazi wa Mosongo wanafuatilia igizo
Thursday, September 21, 2017
Home »
» NURU SANAA NI CHACHU YA MABADILIKO KWA JAMII SERENGETI
0 comments:
Post a Comment