Fahari ya Serengeti

Saturday, September 2, 2017

NG'OMBE ZAIDI YA 385542 KUWEKEWA ALAMA SERENGETI

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akizindua zoezi la uwekaji alama kwa mifugo katika kijiji cha Singisi kata ya Nagusi,amesema wafugaji wataoshindwa kuwekea alama mifugo yao,kusajiri na kuwa na vitambulisho watakuwa wamepoteza sifa za kuwa wafugaji.
Amesema mpango huo unaochangiwa na mfugaji kwa kila ng'ombe sh 500 unalenga kupunguza migogoro kati ya wafugaji ,wahifadhi,wakulima na wawekezaji kwa kuwa utaiwezesha serikali kupata taarifa sahihi za wafugaji na malisho yaliyopo.
 Diwani wakata ya Nagusi Jaksoni Manyeresa akiweka alama ng'ombe
 Afisa mifugo Mesanga naye akiweka alama
 Wananchi wakiwa wanafuatilia maagizo ya serikali ya uwekaji alama
 Wafugaji wanafuatilia kwa makini ili waweze kuanza utekelezaji bila migongano na serikali

 Mjadala

0 comments:

Post a Comment