Fahari ya Serengeti

Thursday, September 7, 2017

MKURUGENZI MUWASA ASIMAMISHWA KAZI

Wizara ya Maji na Umwagiliaji imemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Muwasa Said Gantala baada ya kufikishwa mahakamani na Takukuru kwa tuhuma 15 za kughushi nyaraka na kuchota sh 63,400,000 toka taasisi za fedha za NBC na CRDB Tawi la Musoma.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo Athumani Sharifu amesema Gantala amesimamishwa toka septemba 6 mwaka huu na anatakiwa kumkabidhi meneja Ufundi wa Muwasa na hatatakiwa kutoka eneo la kazi hadi kesi yake iishe. 

0 comments:

Post a Comment