Fahari ya Serengeti

Thursday, September 28, 2017

SAFARI YA KUHAMIA MAJENGO YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERENGETI YAIVA

 Dc Derengeti Nurdin Babu akimweleza Naibu Waziri wa Afya Dk Hamisi Kigwanga mikakati ya ujenzi wa hospitali ya wilaya kupitia wadau mbalimbali kufuatilia serikali kutokutoa fedha za ujenzi toka mwaka 2013/14 ,Hata hivyo Kigwangala ameridhishwa na kasi ya ujenzi na kumtaka mganga mkuu wa wilaya kuhamishia baadhi ya huduma kwenye majengo yaliyokamilika na januari mwaka kesho kazi zianze rasmi katika hospitali ya wilaya.
Amesema wakifanya hivyo watapata fedha za basket Fund,fedha za madawa na vifaa tiba ,miongoni mwa huduma ambazo wameagizwa kuanza nazo ni afya ya uzazi ,kiliniki na matibabu ya nje.
 Karibu Serengeti.
 Ukaguzi unaendelea


 Dk Kigwangala anaangalia jiwe la Msingi lililowekwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu katika hospitali ya wilaya ya Serengeti juni mwaka huu.



0 comments:

Post a Comment