Katika mjadala wa Pamoja viongozi hao wamekubaliana kuwa huduma ya Maji na Umeme ifikishwe eneo hilo ili kurahisisha kazi za ujenzi ambao unatarajiwa kuanza wakati wowote.
Hata hivyo Ded Serengeti Juma Hamsini amemtaka mwekezaji huyo kuchangia gharama za kusambaza maji ili kuharakisha huduma hiyo,kwa kuwa katika bajeti ya Muguwasa hawakuwa na fedha za kupeleka maji eneo hilo zaidi ya kilometa mbili
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mgiye Chacha amesema yuko tayari kuchangia gharama ili kumpunguzia gharama za kufuata maji kisimani
Viongozi wakijadiliana
Rc Mlingwa amesema kazi ya serikali ni kuandaa mazingira wezeshi kwa wawekezaji,hivyo kupeleka maji na umeme ndiyo kazi ya serikali,na kuomba utekelezaji ufanyike kwa haraka.
Mgiye Chacha Mkurugenzi wa Lumuye Leopard Co.Ltd kushoto anasema kutokuwa na maji na umeme wanatumia gharama kubwa na kazi za ufyatuaji matofali inakwenda taratibu.
0 comments:
Post a Comment