Katibu wa wazee wa mila wa koo ya Inchage Muungano wilaya ya Serengeti Yusuph akiwaeleza wakazi wa Omahe kijiji cha Makundusi kuwa walisimamia ukeketaji kwa kutokujua madhara yake,lakini sasa wanasema basi na kuwahimiza kusomesha watoto wa kike ili kujenga Serengeti Mpya isiyo na ukeketaji.
Miongoni mwa kundi lililopokea kwa furaha msimamo wa wazee wa mila kupinga ukeketaji Serengeti ni watoto wa kike ambao kila msimu wa ukeketaji wengi hukimbia makazi ya kwao,sasa wanasema uamzi huo utawawezesha kusoma kwa bidii na kuwataka viongozi wa wilaya hiyo kujenga mabweni kila sekondari ili waweze kukaa shule na kusoma,maana wakati wenzako waliokutangulia wakitembea wewe unatakiwa kukimbia.
Wadau mbalimbali wakitoa ujumbe kitongoji cha Omahe
Sunday, September 24, 2017
Home »
» WAZEE WA MILA WASEMA UKIONA ELIMU NI GHALI JARIBU UJINGA
0 comments:
Post a Comment