Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akikabidhi risala ya Utii kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amour Hamad Amour katika Uwanja wa Mbuzi Mugumu ,kiongozi huyo amewamwagia sifa viongozi na wananchi kutokana na mpangilio mzuri wa mapokezi ya mbio za mwenge wilayani humo.
Amesema mbali na mipangilio mizuri pia miradi yao imetekelezwa kwa kiwango kinachowiana na gharama husika kutokana na ubora,pia jamii ya wakazi wa wilaya hiyo waishio nje ya wilaya wanavyochangia miradi ya kijamii ikiwemo ujenzi wa zahanati ya Busawe,Ofisi ya Kijiji na Bweni la wavulana Ngoreme sekondari.
Makamanda nao hawakuwa nyuma walikaa kwa umoja huku wakihakikisha ulinzi na usalama umeimarika
Brass band toka Tanapa walihanikiza katika mapokezi ya mbio za mwenge
Washiriki wakiwa katika makundi huku wakijjadiliana mambo kadha wa kadha
Makamanda wakiwa imara kabisa kusubiri maelekezo mengine
0 comments:
Post a Comment