Fahari ya Serengeti

Wednesday, November 8, 2017

MARAFIKI WA ELIMU WAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI CHANGAMOTO ZA ELIMU

 Mratibu wa dawati la Jinsia la Polisi wilaya ya Serengeti Paul Pareso akielezea shughuli za dawati la polisi kwa upande wa ukatili wa kijinsia wakati wa mjadala uliowashirikisha wazazi,walezi walimu wa shule ya msingi Mugumu B,ulioandaliwa na Marafiki wa Elimu Serengeti
 Mratibu wa Marafiki wa ELIMU Serengeti Byabato akitoa ufafanuzi wa ushiriki wa Jamii katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kusomea kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Mugumu B,




 Ufafanuzi unatolewa


Monday, November 6, 2017

MRADI WA RAIN WAJENGEA UWEZO KAMATI ZA MAJI ZA KATA YA KENYAMONTA SERENGETI

 Wajumbe wa Kamati za Maji kata ya Kenyamonta wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wanaoendelea na mafunzo ya namna ya kusimamia miradi ya Maji kupitia Mradi wa RAIN unaofadhiliwa na Cocacola Africa Foundation kwa zaidi ya sh 1.4 bil na unatekelezwa na amref health africa-Tanzania katika Kata za Kenyamonta,Mosongo,Nyansurura na Busawe
 Wajumbe wakiwa kwenye mijadala
 wanabadilisha mawazo
 Mwezeshaji akifafanua jambo
Meneja Mradi wa RAIN Mhandisi Japhet Temu kushoto akifuatilia mafunzo ya kamati,kulia ni afisa mtendaji wa kijiji cha Mesaga na katikati ni afisa mtendaji wa kijiji cha Nyagasense Hamisi Mechandi

Saturday, November 4, 2017

KAMPUNI YA JAMBO KUSAIDIA KAMBI YA RIADHA MARA

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo inayotengengeza maji ya Jambo na bindaa nyingine mkoani Shinnyanga Mohammed Abdallah katikati ameahidi kusaidia kambi ya timu ya riadha ya Mkoa wa Mara ambayo itafanyikia wilayani Serengeti.

Katika hafla fupi kwenye bwalo la Polisi Mugumu Serengeti iliyoandaliwa na Chama cha Riadha wilaya ya Serengeti kwa ajili ya wanariadha na viongozi wa mkoa wa Mara baada ya kukamilika kwa mashindano ambayo yameunda timu ya Mkoa ,Mkurugenzi huyo ambaye ameombwa na Dc Serengeti Nurdin Babu kushiriki ameahidi ,kusaidia mahitaji mbalimbali kwa wachezaji kwa kipindi chote cha kambi.

Mkuu wa wilaya hiyo Nurdina Babu amesema ameomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia timu hiyo ambayo inatangaza mkoa wa Mara vema kutokana na jinsi vijana hao wa kike walivyoonyesha vipaji vya hali ya juu.
 Wanariadha,viongozi na wadau wakishiriki  chakula cha pamoja baada ya kumaliza mashindano ya riadha
 Picha ya Pamoja ya viongozi na wanariadha waliofanikiwa kuchaguliwa kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya timu ya mkoa.

Picha ya pamoja



ANASTAZIA MUKAMA AZIDI KUNG'ARA MBIO ZA MITA 10000


Anastazia Mukama mwanafunzi wa kidato cha pili sekondari ya Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara amezidi kung'aa katika riadha baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za mita 10000 kwa kutumia dakika 39 katika mashindano ya riadha mkoa wa Mara yaliyoshirikisha wilaya tatu za Tarime ,Serengeti na Bunda ili kuunda timu ya riadha ya wasichana mkoa wa Mara ambayo itaingia kwenye kinyang'anyiro kitaifa ambapo wataunda timu ya Taifa itakayoshiriki mashindano ya Olimpiki Japan Mwaka kesho.
Katika mashindano ya Rocky City Marathon Anastazia katika mbio za kilometa 5 alikuwa wa kwanza ,haki akiwa amemzunguka mshindani wake 




 Bingwa wa mkoa wa Mara mbio za mita 10000 Jumanne toka Serengeti akipasha mwili joto ikiwa ni maandalizi ya kwenda Kilimanjaro Marathon







TIMU YA RIADHA MKOA WA MARA YAPATIKANA SASA KUINGIA KAMBINI

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Nurdin Babu akitimua mbio mita 100 ikiwa ni uzinduzi wa mashindano ya riadha  kwa wasichana Mkoa huo ambayo yamefanyika Uwanja wa Sokoine Mugumu na kupata jumla ya wakimbiaji 18 wa mbio tofauti wamepatikana.
Wakimbiaji hao kutoka wilaya tatu zilizoshiriki ambazo ni Serengeti ,Bunda na Tarime wataingia kambini kuanzia tarehe 17 mwezi huu kwa ajili ya kunolewa ili kuwapata watano watakowakilisha mkoa kitaifa kwa ajili ya kupata timu ya wasichana wataokwenda Olimpiki Japan Mwaka kesho.
 Baadhi ya wanariadha wakiwa na viongozi kabla ya kuanza mchujo
 Babu amesema wilaya imejipanga kuhudumia wageni kuanzia mashindano hadi kambi ambayo itafanyika wilayani hapo.
 Wanaonyesha makali yao

Mshindi wa kwanza mita 1500

Thursday, November 2, 2017

MRADI WA RAIN TANZANIA WAWAJENGEA UWEZO WATUMIAJI MAJI BUSAWE

Mradi wa RAIN TANZANIA unaofadhiliwa na Cocacola Africa Foundation kwa ajili ya kata nne za wilaya ya Serengeti na unatekelezwa na amref health africa kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Serengeti, umeanza kujengea uwezo kamati ya watumaiji maji wa kata ya Busawe ili kuhakikisha wanasimamia vema mradi huo.


Kamati ya watumiaji maji kata ya Busawe wakijengewa uwezo


 Mwezeshaji akitoa maelekezo kuhusiana na mradi huo unaolenga kuwapatia wananchi maji safi na salama ikiwemo kuwajengea uwezo wa  kiuchumi


 Mnanielewa?mtaalam anawauliza





DIWANI KATA YA STENDI KUU ATAKIWA KUSHIRIKISHA JAMII UKARABATI MUGUMU SEC

 Ded Serengeti Juma Hamsini amemtaka diwani wa kata ya Stendi Kuu kushirikisha wazazi kwa ajili ya kukarabati jengo la utawala la shule ya sekondari Mugumu,
Amesema kwa kuwa watoto wanaosoma hapo ni jamii inayozunguka shule hiyo ni vema kuwashirikisha ili kuchangia nguvu zao kwa lengo la kuboresha mazingira ya kusomea,kujifunzia na walimu kufanyia kazi.

"Diwani naomba uje ofisini kwangu tuangalie namna ya kusaidia tatizo hilo ,lakini naomba ujitahidi kushirikisha jamii kuchangia ,ikizingatiwa kuwa shule hii ni ya mjini inatakiwa kuwa katika mazingira mazuri,"amesema.
 Anasisitiza
Wanafuatilia

MADIWANI WATAKIWA KUBORESHA TAARIFA ZA KATA ZAO

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini katikati,Mkurugenzi Mtendaji Juma Hamsini wa kwanza kushoto na  Makamu Mwenyekiti Pasto Maiso wakipitia taarifa mbali mbali zilizokuwa zinawasilishwa na madiwani katika kikao cha baraza.
Hata hivyo Mwenyekiti amewashauri madiwani kuhakikisha wanaboresha taarifa zao kwa kuzingatia hitaji la kanuni ambayo inawataka kukaa vikao vya kata ikibainisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo,mafanikio ,changamoto na mikakati yao.
 mjadala unaendelea huku madiwani wakifuatilia kwa makini
 Kila mmoja anafuatilia
wanajadiliana

MADIWANI WATAKIWA KUANDIKA KAZI WAZIFANYAZO KILA SIKU

 Meneja wa Mpango wa Maboresho ya serikali za Mitaa Mkoa wa Mara Wakili Mtebe Lusato akiwaelekeza madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti umuhimu wa kuandika kazi zao ambazo wanazifanya na wanazotarajia kuzifanya na mwishoni ifanyike tathimini ya kuona ahadi ,utekelezaji na ambazo hazikutekelezwa kama njia ya kujipima kiutendaji na uwajibikaji kwa wapiga kura
 msisitizo
Wanafuatilia maelekezo

Wednesday, November 1, 2017

RC ATAKA MARA MPYA ISIYO NA UKATILI WA KIJINSIA

 Mkuu wa Mkoa wa Mara Kigoma Ally Malima amewataka wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Mara kuhakikisha wanakomesha matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike.
Akiongea na viongozi  wa wilaya,viongozi wa dini ,vyama vya siasa ,mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti amesema,vitendo vya ukatili wa kijinsia unafanya mkoa huo kuonekana wa ajabu wakati wanaofanya hayo ni watu wachache.

"Naomba kila Dc na kamati ya Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya ukatili hasa ukeketaji ,nataka Mara mpya isiyokuwa na ukatili wa kijinsia,wekeni mikakati ya namna ya kukomesha vitendo hivyo,"anabainisha.


 Dc Nurdin Babu kulia na Ded Juma Hamsini wakijitambulisha

 Rc akijadiliana jambo na watumishi wa idara ya Maendeleo ya Jamii
Wanafuatilia mjadala