Katika hafla fupi kwenye bwalo la Polisi Mugumu Serengeti iliyoandaliwa na Chama cha Riadha wilaya ya Serengeti kwa ajili ya wanariadha na viongozi wa mkoa wa Mara baada ya kukamilika kwa mashindano ambayo yameunda timu ya Mkoa ,Mkurugenzi huyo ambaye ameombwa na Dc Serengeti Nurdin Babu kushiriki ameahidi ,kusaidia mahitaji mbalimbali kwa wachezaji kwa kipindi chote cha kambi.
Mkuu wa wilaya hiyo Nurdina Babu amesema ameomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia timu hiyo ambayo inatangaza mkoa wa Mara vema kutokana na jinsi vijana hao wa kike walivyoonyesha vipaji vya hali ya juu.
Wanariadha,viongozi na wadau wakishiriki chakula cha pamoja baada ya kumaliza mashindano ya riadha
Picha ya Pamoja ya viongozi na wanariadha waliofanikiwa kuchaguliwa kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya timu ya mkoa.
Picha ya pamoja
0 comments:
Post a Comment