MIAKA 20 JELA KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO
Zakaria Wambura(52) Mkazi wa Kijiji cha
Nyansurura wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara amehukumiwa kifungo cha miaka
20 jela kwa kukutwa na meno mawili ya tembo yenye thamani ya Tsh 22.5 milioni.
Akitoa hukumu katika kesi ya Uhujumu Uchumi
namba 106/2016,Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile amesema mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka 20 kutokana
na kosa hilo,ambalo ni kinyume na kifungu cha 86 cha Sheria Namba 5 ya
Wanyamapori ya mwaka 2009.
Mapema Mwendesha mashitaka wa Jamhuri Emmanuel
Zumba ameiambia Mahakama kuwa mshitakiwa
huyo alikamatwa oktoba 29,2016 ndani ya Pori la Akiba la Grumeti,akiwa na
kisu,Shoka ,Panga na meno mawili ya Tembo kinyume cha Sheria.
Ameomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa kuwa
wanyama hao wako hatarini kutoweka,huku mshitakiwa akiomba mahakama kumpunguzia
adhabu kwa kuwa ni kosa lake la kwanza.
0 comments:
Post a Comment