MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA NYAMA KAVU ZA NYUMBU
Mwita Mwikwabe Chacha
(42)mkazi wa kijiji cha Machochwe wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara amehukumiwa
kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kukutwa na vipande 70 vya nyama kavu ya nyumbu
vyenye thamani ya zaidi ya Tsh 56.8 milioni.
Katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 63/2016 Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Ismael Ngaile ametoa adhabu hiyo ili iwe
fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo za kuhujumu mali za Umma.
Mapema Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri Emmanuel Zumba mbele ya Hakimu Ismael Ngaile amesema
kuwa ,aprili 15,2016 mshitakiwa alikamatwa nyumbani kwake Machochwe akiwa na
nyara hizo kinyume cha Sheria.
0 comments:
Post a Comment