Mkuu wa Mkoa wa Mara Kigoma Ally Malima amewataka wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Mara kuhakikisha wanakomesha matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike.
Akiongea na viongozi wa wilaya,viongozi wa dini ,vyama vya siasa ,mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti amesema,vitendo vya ukatili wa kijinsia unafanya mkoa huo kuonekana wa ajabu wakati wanaofanya hayo ni watu wachache.
"Naomba kila Dc na kamati ya Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya ukatili hasa ukeketaji ,nataka Mara mpya isiyokuwa na ukatili wa kijinsia,wekeni mikakati ya namna ya kukomesha vitendo hivyo,"anabainisha.
Dc Nurdin Babu kulia na Ded Juma Hamsini wakijitambulisha
Rc akijadiliana jambo na watumishi wa idara ya Maendeleo ya Jamii
Wanafuatilia mjadala
Wednesday, November 1, 2017
Home »
» RC ATAKA MARA MPYA ISIYO NA UKATILI WA KIJINSIA
0 comments:
Post a Comment