Fahari ya Serengeti

Friday, October 27, 2017

MRADI WA RAIN TANZANIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAJI SAFI NA SALAMA

 Meneja Mradi wa RAIN Mkoa wa Mara Mhandisi Japhet Temu akifafanua utekelezaji wa Mradi wa RAIN ambao unatekelezwa na Amref Health Africa-Tanzania kwa ufadhili wa Cocacola Africa Foundation kwa zaidi ya sh 1.4 bil,Mradi huo utasaidia upatikanaji wa Maji Safi na Salama kwa wakazi wa kata za Mosongo,Kenyamonta,Busawe na Nyansurura ,na utawezesha kiuchumi vikundi 50 vya vijana na 20 vya akina kwa kuwapa mitaji na mafunzo.
Mradi huo unalenga kutatua changamoto za maji safi na Salama,kusambaza maji safi na salama ,kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama karibu na makazi,kujenga vyoo vya kisasa mashuleni,kuhamasisha usafi wa mazingira,kuhamasisha ujengaji na utumiaji bora wa vyoo.
Pia utapunguza magonjwa ya kuhara yanayosababishwa na maji yasiyo safi na salama,kupungua kwa magonjwa ya kichocho yatokanayo na maji machafu.
 Afisa mauzo wa Kampuni  ya Cocacola Shaabani Mshana akitoa ufafanuzi kuhusiana na msaada huo.
 Picha ya pamoja



0 comments:

Post a Comment