Fahari ya Serengeti

Sunday, October 1, 2017

WADAU MBALIMBALI WAJITOKEZA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI



Baadhi ya watalii wa ndani kutoka Mugumu Serengeti wakipata maelezo ya mzunguko wa nyumbu toka mei hadi desemba toka kwa John Elikana mmoja wa wanafunzi wa masomo ya uongoza wageni katika Kituo cha Utalii ndani ya Hifadhi ya Serengeti,wadau hao wa utalii wamesema wataendelea kuhamasisha makundi mbalimbali ya jamii ndani na nje ya wilaya hiyo kufanya utalii wa ndani ambao utasaidia kuinua pato la Taifa.
Serengeti Media Centre ni miongoni mwa wadau walio mstari wa mbele kuhamasisha utalii wa ndani na uhifadhi.
Picha na Serengeti Media.



 Kundi la tembo likiwa limeweka ulinzi mkali kwa watoto wake waliolala chini
 Twiga ni miongoni mwa wanyama vivutio ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
 Wanaangalia viboko na mamba
 Safari kuelelea maeneo mbalimbali inaendelea ,raha ya utalii.
 Eneo hili huwavuta watu mbalimbali
 Viboko wakijivinjali katika anga zao.
 Tembo akihangaika na hali yake
 Wanaelekea eneo lingine huku mjadala ukishika kasi

 Wakisoma maelezo kwenye eneo mahsusi la mawe meupe ambapo wageni hupumzika baada ya kuzunguka na kupata chakula,vinjwaji na hewa safi


 Kuna elimu kubwa kupitia taarifa zilizowekwa ndani ya maeneo tofauti,
 Simba akiwa ametulia kwa uzuri
 maelezo yanatolewa
 Watalii wa nje nao hawakuwa nyuma kupata taarifa katika kituo cha utalii Serengeti
 Mzunguko unaendelea
 Hata hawa wanyama ni kivutio kikubwa hasa nyumbu kutokana na maisha yao,huvuta wageni toka kona zote za dunia,raha ya Hifadhiya Serengeti hiyo.

 Taarifa za mafuvu zinazidi kukonga nyoyo za watalii wa ndani

 Hatimaye wanatua kwenye Picha ya Hayati baba wa Taifa na rafiki yake


0 comments:

Post a Comment