Fahari ya Serengeti

Tuesday, October 24, 2017

VIONGOZI LINDENI VYANZO VYA MAJI


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilayaya Serengeti Mhandisi Juma Hamsini amesema chanzo cha Maji cha Bwawa la Manchira kiko hatarini kuharibika kutokana na viongozi kwa kushirikiana na wananchi kuchungia mifugo katika eneo hilo.
Amemwomba mkuu wa wilaya kutumia vyombo vyake kuwakamata watu wanaohujumu chanzo hicho kwa kupeleka mifugo kwa kuwa athari zake ni kubwa kwa jamii na serikali.
Hamsini amesikitishwa pia na miradi mbalimbali iliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kutokufanya kazi kutokana na misimamo isiyokuwa na tija ya baadhi ya viongozi na wengine kushindwa kutoa mafuta ya uendeshaji na kusababisha wananchi kuhangaika kutafuta maji umbali mrefu.
 Anasisitiza
 Wanafuatilia




0 comments:

Post a Comment