Fahari ya Serengeti

Thursday, October 26, 2017

KUEPUKA MAJANGA YA MOTO WASHAURIWA KUFUNGUA AKAUNTI

 Meneja wa NMB Tawi la Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara akielezea wanafunzi wa sekondari ya Serengeti umuhimu wa kufungua akaunti ili kuepukana hasara za kutunzia ndani fedha inapotokea majanga.
Oktoba 26 mwaka jana bweni la wasichana wa shule hiyo liliteketea kwa moto na kuteketeza vitu vyote ikiwemo fedha ambazo walikuwa wametunzia ndani.
Katika hafla ya kukabidhi mabati 185 kwa ajili ya shule hiyo na madawati 50 kwa ajili ya shule ya Msingi Tamukeri,msaada huo ukiwa na thamani ya sh 10 mi,amesema NMB ina akaunti mbalimbali hivyo wanafunzi wanaruhusiwa kufungua akaunti kwa ajili ya usalama wa fedha zao na kudhibiti matumizi yasiyokuwa ya lazima.




0 comments:

Post a Comment