Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nudin Babu ameagiza kushughulikiwa kwa watu wanaoharibu vyanzo vya maji na kusababisha shida kwa wananchi.
Akizindua Mradi wa Replenish Africa Initiative (RAIN) Unaofadhiliwa na Coca cola Africa Foundation na unatekelezwa na amref health africa Tanzania kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Serengeti kwa zaidi ya sh 1.4 bilioni na utakelezwa katika kata nne za Mosongo,Busawe,Kenyamonta na Nyansurura na watu zaidi ya 66513 watanufaika na mradi huo.
Amewaonya viongozi wa kisiasa kutotimua nafasi za kupotosha watu badala wawe watatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi ikiwemo kuwashirikisha wananchi na kuwadhibiti ambao wanaojihusisha na uharibifu wa miradi ya maji.
Wanafuatilia taarifa mbalimbali za mradi wa Maji wa RAIN
Das Serengeti Cosmas Qamara akisisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji
0 comments:
Post a Comment