Fahari ya Serengeti

Sunday, September 10, 2017

HONGERA KWA KUHITIMU



Mama na Mwana wakiwa viwanja vya Sekondari Twibhoki wakati wa Mahafali ya darasa la saba na kidato cha nne ambayo Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu amesisitiza kusomesha watoto wa kike.




Zawadi mbalimbali ikiwemo keki zimetawala katika viwanja hivyo


 Mmabo yanaendelea
 Ilifika wakati wa watoto kutoa zwadi kwa wazazi


SAFARI MOJA HUANZISHA NYINGINE,HONGERA KWA

 Ashukuriwe Bwana wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa Neema zake juu ya Mwanetu Swetbetha kuhitimu darasa la saba shule ya awali,Msingi na Sekondari Twibhoki,hapo akipokea Chake toka kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu,safari moja inaanzisha nyingine naamini atafikia malengo yake,Mungu zidi kumuimarisha katika kusaka maarifa na hekima,na wazazi wake pia waweze kumwezesha kufikia hatua hiyo.Tumrudishie nini Bwana kwa Ukarimu wake.
 Mama na Mwana katika viwanja vya Sekondari ya Twibhoki,hongera sana
 Sweetbertha kushoto na marafiki zake
 Mama akimpa zawadi ya keki mwanae ikiwa ni ishara ya Upendo na kumtakia mafanikio makubwa katika safari yake ya kusaka elimu.
 Dada akimlisha mdogo wake keki akimpongeza kwa kuhitimu darasa la saba na kumtakie heri katika safari nyiingine ya masomo ya sekondari
 Hongereni
 Anazidi kupongezwa
 Wazazi na wageni waalikuwa wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mahafali
 Hongera sana
Hongereni sana

Saturday, September 9, 2017

CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU

Gari lililobeba wasanii wa Nuru Sanaa ,wazee wa mila na baadhi ya viongozi w,
akisukuma gari lao baada kukwama katikati ya kijiji cha Bonchugu na Kisangura wilayani ya Serengeti  wakati wakitoka kwenye mkutano wa wazee wa mila kijiji cha Bonchugu ambao uliitishwa ili kutoa msimamo wao wa kupiga marufuku ukeketaji,kushoto gari la fuso likiwa limekwama.
Hata hivyo imebainika utengenezaji wa barabara katika eneo hilo unatakiwa kutazamwa upya kutokana na ubovu wake.
Kila mmoja na staili yake

 Msafiri kakiri ndivyo inavyoonekana hapo wanapambana kulikwamua gari hakuna mtu mme wala mtu mke wote ni kazi
Umoja ni nguvu hatimaye wakajikwamua

WATAALAM TIMIZENI WAJIBU KUNUSURU AFYA ZA WALAJI

 Mkazi wa kijiji cha Bonchugu wilaya ya Serengeti akiuza nyama katika mazingira hatarishi,licha ya wataalam wa afya na watendaji wa serikali kuwepo katika eneo hilo hakuna hatua zinazochukuliwa ili kulinda afya za walaji.

Mbwa wananyemelea nyama katika bucha ya mkazi mmoka wa kijiji cha Bonchugu wilayani Serengeti

Friday, September 8, 2017

IGIZO LA SANAA NURU KUHUSU ATHARI ZA UKEKETAJI LAWALIZA WAKAZI WA BONCHUGU SERENGETI

 Wasanii wa Sanaa Nuru toka Mugumu Serengeti wakitoa elimu juu ya athari za ukeketaji katika kijiji cha Bonchugu wilayani hapo,kutokana na ujumbe wake wenye hisia baadhi ya akina mama walitokwa machozi wakidai wakati wanakeketwa hawakujua madhara yake bali walikuwa wakitimiza mila na desturi na kwa sasa hawako tayari kuwafanyia watoto wao wa kike,

 Wanafuatilia igizo
 Wazee wa mila wa Koo ya Inchugu na baadhi ya viongozi wakifuatilia igizo

SOKO LA KUKU LINAZIDI KUSHAMIRI MAENEO MENGI SERENGETI

 Wakazi wa kijiji cha Bonchugu wilaya ya Serengeti wakisubiri kuku wanaopelekwa katika soko kwa ajili ya kununua na kwenda kuuza mjini Mugumu,soko la kuku wa kienyeji linazidi kushamiri hasa kipindi hiki cha msimu wa utalii ambapo jogoo anauzwa kati ya sh 15,000- 20,000



Thursday, September 7, 2017

WAZEE WA INCHAGE WAJITOKEZA HADHARANI KUPINGA UKEKETAJI

Mwenyekiti wa Koo ya Inchage Muungano Sungura toka Mbalibali akielezea sababu za wazee wa mila kupiga marufuku ukeketaji wa watoto wa kike katika kijiji cha Kisangura wilaya ya Serengeti,na kuwataka wazazi kusomesha watoto wa kike kwa kuwa mila hiyo ni chanzo cha ndoa za utotoni na kuwakandamiza watoto wa kike.
Amesema kwa makubaliano ya wazee wa mila wa koo sita wilayani hapo walioweka saini mbele ya mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu kupitia Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref healtth africa ,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)halmashauri na wadau wengine kwa ufadhili wa UN WOMEN.
Amesema kutokana na makubaliano hayo kila wazee wa koo wanatakiwa kwenda kuongea na jamii yao kupitia mikutano ya hadhara kwa kuwa wazee wa mila ndiyo wanadaiwa kusimamia zoezi la ukeketaji.

Wakazi wa kijiji cha Kisangura wakiwasikiliza wazee wa mila wa koo ya Inchage wakielezea msimamo wao wa kupinga ukeketaji.
Afisa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti William Mtwazi mwenye karatasi akiongea na wazee wa mila wa kata ya Kisangura kabla ya kuanza mkutano wa hadhara,mwenye shati jekundu ni Meneja wa Mradi huo Godfrey Matumu.
Afisa tarafa ya Ikorongo Paul Shanyangi akitoa msimamo wa serikali kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Nurdina Babu kuhusiana na ukeketaji.

Balozi

MKURUGENZI MUWASA ASIMAMISHWA KAZI

Wizara ya Maji na Umwagiliaji imemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Muwasa Said Gantala baada ya kufikishwa mahakamani na Takukuru kwa tuhuma 15 za kughushi nyaraka na kuchota sh 63,400,000 toka taasisi za fedha za NBC na CRDB Tawi la Musoma.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo Athumani Sharifu amesema Gantala amesimamishwa toka septemba 6 mwaka huu na anatakiwa kumkabidhi meneja Ufundi wa Muwasa na hatatakiwa kutoka eneo la kazi hadi kesi yake iishe. 

Monday, September 4, 2017

KIKUNDI CHA NURU SANAA CHATOA ELIMU YA UNYAGO BILA UKEKETAJI

Wasanii wa Nuru sanaa kutoka Mugumu wilaya ya Serengeti wakitoa elimu ya Unyago bila Ukeketaji katika kijiji cha Kebanchabancha kwa kushirikiana na Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti,wamewakuna wazee wa mila na wananchi ambapo bila ajizi wametoa tamko la kukomesha ukeketaji huku wakiwaambia wafanye unyago bila ukeketaji,tamko hilo la wazee wa mila wa koo ya Inchugu limkoleza elimu iliyotolewa na wasanii hao baada ya kuonyesha faida za Unyago bila ukeketaji na madhara ya ukeketaji.
 Wasanii wakitoa elimu kwa njia ya sanaa,ama hakika zama zimebadilika ,wazee wa mila na wananchi wamesema ukeketaji si dili ,mpango mzima kwa sasa ni Unyago bila ukeketaji.

Kila jambo na watu wake ,hakika wasanii wa Nuru Sanaa Serengeti ni zaidi ya wasanii kutokana na kuvaa uhusika na kufikisha ujumbe kwa jamii.

KAMPUNI YA LUMUYE LEOPARD.CO.LTD KUANZA UJENZI WA KIWANDA


Mkurugenzi wa Kampuni ya Lumuye Leopard Co.Ltd ya Mugumu wilaya ya Serengeti Mgiye Chacha akisaidiana na mafundi kupanga matofali yanayofyatuliwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha Kukamua mafuta ya alizeti eneo la Tambisa Mugumu Serengeti,Kiwanda hicho kinachotarajia kugharimu zaidi ya sh 2.2 bil kinatarajia kutoa ajira 700 zilizo rasmi na zisizorasmi ikiwa ni mikakati ya utekelezaji wa sera ya Viwanda.
 Ufuatuaji wa matofali unaendelea ili kuhakikisha yanafika zaidi ya 50,000
 Kazi ni kazi vijana wanatengeneza fedha kwa kazi ya kufyatua matofali.