Fahari ya Serengeti

Friday, October 27, 2017

MRADI WA RAIN TANZANIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAJI SAFI NA SALAMA

 Meneja Mradi wa RAIN Mkoa wa Mara Mhandisi Japhet Temu akifafanua utekelezaji wa Mradi wa RAIN ambao unatekelezwa na Amref Health Africa-Tanzania kwa ufadhili wa Cocacola Africa Foundation kwa zaidi ya sh 1.4 bil,Mradi huo utasaidia upatikanaji wa Maji Safi na Salama kwa wakazi wa kata za Mosongo,Kenyamonta,Busawe na Nyansurura ,na utawezesha kiuchumi vikundi 50 vya vijana na 20 vya akina kwa kuwapa mitaji na mafunzo.
Mradi huo unalenga kutatua changamoto za maji safi na Salama,kusambaza maji safi na salama ,kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama karibu na makazi,kujenga vyoo vya kisasa mashuleni,kuhamasisha usafi wa mazingira,kuhamasisha ujengaji na utumiaji bora wa vyoo.
Pia utapunguza magonjwa ya kuhara yanayosababishwa na maji yasiyo safi na salama,kupungua kwa magonjwa ya kichocho yatokanayo na maji machafu.
 Afisa mauzo wa Kampuni  ya Cocacola Shaabani Mshana akitoa ufafanuzi kuhusiana na msaada huo.
 Picha ya pamoja



Thursday, October 26, 2017

KUEPUKA MAJANGA YA MOTO WASHAURIWA KUFUNGUA AKAUNTI

 Meneja wa NMB Tawi la Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara akielezea wanafunzi wa sekondari ya Serengeti umuhimu wa kufungua akaunti ili kuepukana hasara za kutunzia ndani fedha inapotokea majanga.
Oktoba 26 mwaka jana bweni la wasichana wa shule hiyo liliteketea kwa moto na kuteketeza vitu vyote ikiwemo fedha ambazo walikuwa wametunzia ndani.
Katika hafla ya kukabidhi mabati 185 kwa ajili ya shule hiyo na madawati 50 kwa ajili ya shule ya Msingi Tamukeri,msaada huo ukiwa na thamani ya sh 10 mi,amesema NMB ina akaunti mbalimbali hivyo wanafunzi wanaruhusiwa kufungua akaunti kwa ajili ya usalama wa fedha zao na kudhibiti matumizi yasiyokuwa ya lazima.




Wednesday, October 25, 2017

NMB BENKI YATATUA TATIZO LA WANAFUNZI TAMUKERI KUKAA CHINI

 Meneja wa NMB Benki Kanda ya Ziwa Abraham Agostino kulia akimkabidhi Katibu Tawala wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara madawati 50 yenye thamani ya sh milioni 5 kwa ajili ya shule ya Msingi Tamukeri kata ya Mbalibali,ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.
 Viongozi wakiwa wanajadiliana mambo mbalimbali meza kuu
 Wanafunzi serengeti sec




NMB BENKI YAIKUMBUKA SERENGETI SEKONDARI

Meneja wa NMB Benki Kanda ya Ziwa Abraham Agostino kushoto akikambidhi Katibu Tawala wilaya Serengeti Cosmas Qamara mabati 185 yenye thamani ya sh milioni 5 kwa ajili ya shule ya sekondari Serengeti ,ikiwa ni sehemu ya kusaidia huduma za jamii kama elimu na afya na kurudisha faida yake kwa jamii.
Wanakagua maeneo mbalimbali ya shule kabla ya makabidhiano.
Katibu Tawala kushoto akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Serengeti sekondari Raymond Nyamasagi.
Meneja wa Kanda NMB Benki akitoa nasaha kwa wanafunzi wa serengeti sec kuishika elimu
Wanafuatilia maelekezo toka kwa viongozi.
Wanasoma risala

Das akitoa nasaha

Tuesday, October 24, 2017

WADAU WASHIRIKI KWENYE ZOEZI LA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI

 Picha ya wadau walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa RAIN wilaya ya Serengeti unaofadhiliwa na Cocacola Africa Foundation kwa zaidi ya sh 1.4 bil
 Uzinduzi umefanyika
Afisa mauzo wa Cocacola Mkoa wa Mara Shaaban Mshana katikati akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Hamsini kulia

IMARISHENI UMOJA KATIKA KUTEKELEZA MIRADI YA JAMII

 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa amref health africa Tanzania Mhandisi Mturi James amewataka viongozi kutumia lugha zinazowaleta pamoja wananchi wakati wa uutekelezaji na kuondoa tofauti za kisiasa ambazo zinaweza kuwa kikwazo na kusababisha adha kwa wananchi.
Katika uzinduzi wa mradi wa RAIN unaofadhiliwa na Cocacola  Africa Foundation kwa zaidi ya sh 1.4 katika vijiji 15 kwenye kata nne za Mosongo,Busawe,Kenyamonta na Nyansurura amesema,viongozi wanatakiwa kuachana na lugha za kuwabagua watu kwa mtizamo wa kisiasa kwenye mambo yenye maslahi ya jamii.
"Mkitumia vema siasa mnaweza kuwaunganisha wananchi pamoja na pia mnaweza kuwagawa watu kwa mitizamo ya kisiasa ,binafsi huwa sipendi sana lugha za wanasiasa ,hii inaweza kukwamisha ama kufanikisha miradi kama mtaitumia vizuri,"anasema.
 Anasisitiza.


Ufafanuzi unatolewa

VIONGOZI LINDENI VYANZO VYA MAJI


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilayaya Serengeti Mhandisi Juma Hamsini amesema chanzo cha Maji cha Bwawa la Manchira kiko hatarini kuharibika kutokana na viongozi kwa kushirikiana na wananchi kuchungia mifugo katika eneo hilo.
Amemwomba mkuu wa wilaya kutumia vyombo vyake kuwakamata watu wanaohujumu chanzo hicho kwa kupeleka mifugo kwa kuwa athari zake ni kubwa kwa jamii na serikali.
Hamsini amesikitishwa pia na miradi mbalimbali iliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kutokufanya kazi kutokana na misimamo isiyokuwa na tija ya baadhi ya viongozi na wengine kushindwa kutoa mafuta ya uendeshaji na kusababisha wananchi kuhangaika kutafuta maji umbali mrefu.
 Anasisitiza
 Wanafuatilia




Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nudin Babu ameagiza kushughulikiwa kwa watu wanaoharibu vyanzo vya maji na kusababisha shida kwa wananchi.
Akizindua Mradi wa Replenish Africa Initiative (RAIN) Unaofadhiliwa na Coca cola Africa Foundation na unatekelezwa na amref health africa Tanzania kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Serengeti kwa zaidi ya sh 1.4 bilioni na utakelezwa katika kata nne za Mosongo,Busawe,Kenyamonta na Nyansurura na watu zaidi ya 66513 watanufaika na mradi huo.
Amewaonya viongozi wa kisiasa kutotimua nafasi za kupotosha watu badala wawe watatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi ikiwemo kuwashirikisha wananchi na kuwadhibiti ambao wanaojihusisha na uharibifu wa miradi ya maji.
 Wanafuatilia taarifa mbalimbali za mradi wa Maji wa RAIN


Das Serengeti Cosmas Qamara akisisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji

Saturday, October 21, 2017

MBUNGE RYOBA ASEMA MFUKO WA JIMBO UNAENDESHWA KWA UWAZI

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba amesema fedha za mfuko wa jimbo zinatumika kwa uwazi na zimesaidia kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo na taarifa yake inatolewa kwa wananchi hadharani ikiwa ni tofauti na ilivyokuwa.
Akihutubia mkutano wa hadhara uwanja wa mbuzi amesema ataendelea kuwajulisha wananchi matumizi yake na kuwataka madiwani wote wa Chadema kufanya kazi kwa uwazi na kuwapa wananchi taarifa.
 Wananchi wakiwa wamejipanga mstari kwa ajili ya kuuliza au kutoa kero kwa mbunge wa Jimbo la Sreengeti Marwa Ryoba
 Viongozi wakijadiliana
Baadhi ya wananchi wafuatilia mkutano

Tuesday, October 17, 2017

MARAFIKI WA ELIMU WADAI RUZUKU HAITUMIKI KAMA ILIVYOPANGWA

 Wadau wa elimu wakifuatilia mrejesho wa Ufuatiliaji wa Marafiki wa Elimu wilaya ya Serengeti juu ya Matumizi ya Fedha za umma kwa shule za Msingi 15 na kumi za sekondari ambapo wamedai fedha za ruzuku na fidia ya ada hazitumiki kwa kazi husika,na utunzaji wa kumbukumbu za fedha ni mbovu.
 Afisa Tarafa ya Grumeti Paul Shanyangi akisisitiza jambo kwa wadau wa elimu kabla ya Marafiki wa elimu hawajatoa mrejesho wao.
 Wanafuatilia
 wanasikiliza kwa makini