Fahari ya Serengeti

Thursday, June 16, 2016

WATENDAJI WA KATA NA MAAFISA TARAFA SERENGETI WAWEKA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA UKEKETAJI

 Afisa mtendaji wa kata ya Mchochwe wilayani Serengeti akiwasilisha mikakati ya namna ya kutokomeza ukeketaji,miongoni mwa njia hizo ni kutoa elimu ,kukutana na makundi ya wazee wa mila na ngariba,vyombo vya dola kusimamia sheria zilizopo zinazoharamisha ukatili huo unaofanywa kwa watoto wa kike.Kupitia Mradi wa Amref kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)wadau mbalimbali wameshirikishwa ili kuhakikisha kila mmoja anafikiwa kuelezwa madhara ya ukeketaji kiafya na kisaikolojia.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kutoka kwa wawezeshaji,wilaya ya Serengeti na Tarime zinatajwa kuwa vinara wa ukeketaji katika mkoa wa Mara,na mwaka huu ukeketaji unatarajiwa kufanyika ,na inasemekana vikao vya maadalizi vya wazee wa mila vinaendelea ikiwa nji pamoja na kupanga viwango watakavyotozwa watoto wanaokeketwa.
 Watendaji wa kata wakisikiliza mada kwa utulivu .
 Mada zinaendelea
 Mmoja wa wawezeshaji akiwa akisoma moja ya visa mkasa kutoka kwenye simu yake.
 Tunaffuatilia mada zinazotolewa wanaonekana wakisema washiriki wa mafunzo.
 Afisa Tarafa ya Grumeti Paul Shanyangi akitoa maelezo ya namna ya kufanya ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linachangia madhara kwa watoto wa kike.


 William Mtwazi afisa mradi wa Tokomeza Ukeketaji kutoka LHRC akitoa ufafanuzi wa namna ya utekelezaji wa mradi huo kwa kushirikisha makundi mbalimbali ya kijamii wilayani serengeti.
 Tulipo Tumekufikia hapa washiriki wakiwa kwenye makundi wakijadili mada na kuweka mikakati ya nini kifanyike ili kukabiliana na ukatili wa kijinsia ikiwemo ni pamoja na ukeketaji.
 Uwasilishaji kimakundi ukiendelea.
 Anachangia kwa hisia kali kutokana na ukatili wa mtoto wa kike anavyofanyiwa ukatili bila ridhaa yake,kukeketwa kwa kuwa wanapata madhara makubwa wakati wa kujifungua,kuchanika ,kuvuja damu nyingi na vifo wakati wa ukeketaji.

 Mwezeshaji wa mada ya Haki za Binadamu Samwel Mewama akitimiza Haja.
 Burudani wakati mwingine ziliztumika kuweka darasa sawa.

 Mganga mkuu wa wilaya Salum Manyatta akiwasilisha mada ya madhara ya ukeketaji kiafya.
 Wawezeshaji wakiwa wanajadiliana kwa pamoja
 Kazi za makui zikiendelea.

0 comments:

Post a Comment