Fahari ya Serengeti

Tuesday, June 14, 2016

KERO ZA WAFANYABIASHARA HASA SOKO KUU LA MUGUMU SERENGETI


 Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Naomi Nnko akisalimia wafanyabiashara wakati wa kikao kilichowakutanisha viongozi wa wilaya na wafanyabiashara ambapo miongoni mwa kero zilizowasilishwa ni upandishaji wa gharama za meza kutoka sh 2,500 hadi 15,000 kwa mwezi na vibanda kutoka 40,000 hadi 150,000 kwa mwezi,kutokutengeneza soko eneo la kuuzia vyakula,dagaa na matunda,kutokudhibiti mbuzi wanaoingia ndani ya soko hilo.
 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Juma Porini akijibu kero za wafanyabiashara
 Baadhi ya wauza mboga ,matunda na wafanyabiashara wa mji wa Mugumu wakiwa wamekaa wakifuatilia kikao.
 Makundi mbalimbali yalishiriki kwenye mkutano huo.
 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Maftah Ally akijibu na kutoa ufafanuzi wa kero mbalimbali zilizowasilishwa na wafanyabiashara.

1 comment:

  1. Serengeti media centre ndicho kituo pekee kinachoijuza jamii uharisia wa mambo hongera sana

    ReplyDelete