Fahari ya Serengeti

Thursday, June 16, 2016

VIONGOZI WA MADHEHEBU SERENGETI WAAHIDI KUSAIDIA KUELIMISHA WAUMINI WAO KUTOKOMEZA UKEKETAJI.

 Ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia hususan ukeketaji wa watoto wa kike wilayani Serengeti kupitia Mradi wa Tokomeza Ukeketaji unaotekelezwa na mashirika ya Amref na LHRC kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali,Viongozi wa madhehebu wilayani hapa wameahidi kutumia nafasi zao kufikisha ujumbe kwa jamii kwa kuwa madhara yake yanazidi kuwa makubwa kwa wasichana ikiwemo ndoa za utotoni kwa kuwa kukeketwa kunachukuliwa kama kipimo cha kukua ,na inaathiri maendeleo ya mtoto wa kike kielimu,na huoni mwendelezo wa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali juu ya madhara ya ukeketaji.
 Meneja Mradi wa Amref Godfrey Matumu akiwaeleza viongozi wa madhehebu malengo ya mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti ,viongozi hao ni sehemu ya wadau wa utekelezaji wa mradi huo ili kupunguza madhara yanayowakutana watoto wa kike wakati wa ukeketaji na baada ya hapo.hasa wakati wa kujifungua.
 Afisa Mradi wa Tokomeza Ukatili Serengeti toka LHRC William Mtwazi akichangia mada wakati wa mafunzo juu ya ukatili wa kijinsia kwa viongozi wa madhehebu wilayani humo ambao ni miongoni mwa wadau watakaohusika kusambaza elimu juu ya madhara ya ukatili huo.
 Viongozi mbalimbali wa madhehebu wakiwa wanaendelea na mafunzo juu ya athari za ukeketaji na ukatili wa kijinsia .
 Wanafuatilia mada mbalimbali.
 Kila mmoja anaandika mambo ya msingi ili ambayo yatamsaidia kutoa elimu kwa waumini wake kuhusiana na madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike
 Mjadala mpana ulipewa nafasi wakati wa kazi za vikundi ambao ulisaidia kujua ukubwa wa tatizo na namna ya kukabiliana na hali hiyo.
 Mijadala inaendelea
 Kazi na dawa watoa huduma ya chakula nao walishirikishwa kwenye mjadala mpana ili watambue madhara ya ukeketaji,kwa kuwa Kila ulipo utafikiwa na elimu hii ili kuwanusuru watoto wa kike.
 Mjadala ulishirikisha jinsi zote njia ambayo imesaidia kujua kwa undani madhila wanayopata watoto wa kike wanapofanyiwa ukatili huo,ikiwemo kiafya,kielimu,kisaikolojia na kiimani.

 Mmoja wa viongozi wa dini akiwasilisha mada ikiwa ni kazi ya vikundi na mapendekezo yake.
 Mtoa mada ya Ukatili wa Kijinsia Hidaya Mkaruka kutoka Ofisi ya Maendeleo ya jamii wilaya akiandika maoni ya washiriki kadri walivyokuwa wakichangia.
 Anamwaga nondo.
 Mchungaji Maalim Lazaro wa kanisa la Sayuni akiwasilisha kazi ya vikundi juu ya athari za ukatili wa kijinsia.
Amani Muhango akiwasilisha kazi ya kikundi chao.

0 comments:

Post a Comment