MBEGU KINZANI ZASAIDIA KUTOKOMEZA
GUGU LA KIDUHA,
Serengeti Media Centre Media.
Wakulima wa
kata nane wilayani hapa wameanzisha kampeini ya kutokomeza gugu hatari la
Kiduha ambalo limekuwa likiathiri uzalishaji wa zao hilo la chakula na
biashara.
Kata hizo ni
pamoja na Rung’abure,,Manchira,Morotonga,Nyamoko,Uwanja wa
ndege,Geitasamo,Mbalibali na Machochwe.
Gugu hilo
ambalo inadaiwa kusambaa kwa kasi na kuathiri ukuaji na uzalishaji wa zao la
mahindi ,inadaiwa mbegu zake hukaa chini kwa zaidi ya miaka 15 bila kuota na
limeathiri wakulima katika nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Akitoa
ufafanuzi wa kampeini hiyo Mratibu wa Kampuni ya African Agricultural
Technology Foundation (AATF)yenye makao makuu yake jijini Nairobi Nchini Kenya na Ofisi ndogo jijini Mwanza,
Jovita Joachim wakati wa sherehe ya Mkulima katika kijiji cha Rung’abure jana
,alisema kutokomezwa kwa gugu hilo kutaongeza uzalishaji na kipato kwa
wakulima.
“Gugu la
Kiduha ni hatari sana maana mche mmoja huzalisha mbegu 40 hadi 50 milioni ,na
husambaa kwa njia nyingi ikiwemo mifugo,watu na wakati mwingine upepo…na
limechangia wakulima wengi kukata tamaa kutokana na uzalishaji mdogo
wanaopata,”alisema.
Alisema
baada ya utafiti wa makampuni mbalimbali duniani ulibaini mbegu ya (Meru
IR621)ina uwezo wa kutokomeza gugu hilo kutokana na viwatilifu vyake na
huongeza uzalishaji mahindi kwa ekari moja hadi magunia 24 kwa kuwa inaua nguvu ya gugu hilo
ambalo hufyonza maji chini ya mmea na uharibu rutuba ya ardhi.
Baadhi ya
Mikoa ambayo imeathiriwa na gugu hilo ni pamoja na
Tanga,Pwani,Lindi,Mtwara,Dodoma,Iringa,Mbeya,Ruvuma,Mwanza na Mara ,na kwa
kanda ya ziwa wilaya za Serengeti,Butiama,Musoma,Rorya,Misungwi,Magu,Kwimba,Bunda,Rorya
na Butiama.
Kwa Upande
wake Mkuu wa wilaya hiyo Maftah Ally aliwataka wakulima kuacha kilimo cha mazoea na kwa kutumia teknolojia hiyo watafanikiwa
kutekeleza kampeini iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa huo Magesa Mulongo ya
kujilisha mwenyewe.
“Hakuna haja
ya kuhitaji msaada wa chakula kwa wakazi wa wilaya hii kwa kuwa mvua toka
agosti mwaka jana hadi sasa inanyesha,tumieni teknolojia ya kisasa ili muongeze
mavuno na soko lipo kwa kuwa kuna viwanda vya kusaga unga vinafunguliwa
wilayani humo,”alisema.
Akizungumzia
mafanikio ya teknolojia hiyo Tatu Nyamuronga mkulima kutoka kijiji cha Miseke
alisema yeye ameweza kupata magunia 27 kwa ekari moja ,wakati awali alikuwa
akivuna magunia 5hadi 7.
Naye Magoiga
Nyamuhanga mkulima kutoka Rung’abure alishauri elimu itolewe zaidi kwa kuwa
wakulima walikuwa wakitilia shaka mbegu
kutoota.
Mwisho.
Baadhi ya maafisa wa kilimo wakielezea athari ya gugu la kiduha kwa zao la mahindi.
Baadhi ya wakulima wakiangalia mahindi katika moja ya shamba la mkulima wa kijiji cha Rung'abure.
Burudani mbalimbali zilikuwepo ikiwemo chakula na vinywaji.
0 comments:
Post a Comment