MIFUGO ICHANGIE MAENDELEO YA WATOTO
KIELIMU,
Serengeti Media Centre
Jamii ya
wafugaji wilayani hapa Mkoa wa Mara inatakiwa kubadili mitizamo kwa kutumia
rasilimali walizonazo kusomesha watoto wao hasa wa kike badala ya kuwaoza.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini alisema hayo wakati wa
harambee ya kuchangia madawati katika kata ya Kyambahi kwa ajili ya shule za
msingi tatu zinazokabiliwa na upungufu wa madawati 174.
Alisema
sekta ya mifugo inahitaji wasomi na wataalam mbalimbali ambao watasaidia sekta
hiyo kutoa matunda mazuri,lakini baadhi ya
wafugaji wameshindwa kuwekeza
kwenye elimu ya watoto wao ambao watasaidia kusukuma maendeleo ya taifa.
“Wazazi
hakuna sababu ya kuwatupia lawama walimu juu ya kutofaulu kwa watoto kwenye masomo yao,chanzo ni ninyi wenyewe kutokuona
umuhimu wa kuchangia elimu na kuwaendeleza watoto,kuendelea na tabia hiyo
kutalikosesha taifa wasomi …wafugaji utajiri wenu wa mifugo utumike kuleta
mabadiliko kwenye familia zenu na jamii ,wekezeni kwenye elimu ndiyo faida
isiyokwisha thamani,”alisema.
Akiongoza
harambee hiyo iliyolenga kubata madawati 174 yenye thamani ya zaidi ya sh 2
milioni, na kufanikiwa kupata sh 5,124.200 ikiwa fedha taslimu sh3031200, ahadi
sh2,093,000, madawati 105 ahadi ngombe
3,mbuzi 4,Meya wa Manispaa ya Musoma William Gumbo alisisitiza wananchi kuwa
mstari wa mbele kuchangia maendeleo yao.
“Ni wajibu
wa wazazi kuandaa watoto wao kielimu ili waweze kupata mwanga wa kusaidia
jamii,hakuna mtu atakuja kuwasomeshea watoto wenu hilo ni jukumu la kila
mzazi,kwa kufanya hivyo mnawaandaa pia kuja kuwa wazazi bora,”alisema.
Gumbo pamoja
na kuchangia madawati 10 na kuwasilisha mchango wa madawati 50 ya mbunge wa
Musoma mjini Vedastus Mathayo ambaye amewekeza katika kijiji hicho,aliwataka
kuachana na dhana potofu kuwa serikali itafanya kila kitu kwa msingi wa elimu
bure,bali wazazi wanawajibu pia.
Mapema Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Kyambahi Mukome Manyanya na Mratibu elimu kata Nemes Sianga
wakitoa taarifa zao walisema mbali na upungufu wa madawati kata hiyo haina
shule ya sekondari hali inayochangia utoro kwa kuwa baadhi ya wanafunzi
wanatembea zaidi ya saa 4 kufika shuleni.
Walisema
moja ya mkakati walionao kwa kushirikisha jamii ni kujenga shule ya sekondari
ili kuwapunguzia safari ndefu wanafunzi,hali ambayo pia itachangia mazingira
rafiki ya kusoma.
Ili
kuhakikisha wilaya hiyo inakamilisha upungufu wa madawati zaidi ya 14,000 kwa
shule za msingi na sekondari ,kila kata imepewa jukumu la kutatua matatizo
yaliyopo,na wilaya inawaongezea kila kata madawati 20.
Mwisho.
Baadhi ya viongozi wa kata,tarafa,kijiji na wilaya wakiwa wamekaa wakisubiri utaratibu.
Mwenyekiti wa Manispaa ya Musoma William Gumbo akiwa anafungua baadhi ya michango ya wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya kata hiyo ambapo yeye na mbunge wa Musoma mjini walichangia madawati 60.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Naomi Nnko akisisitiza umuhimu wa jamii kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment