Wanafuatilia michezo na hotuba
Wanafunzi wa shule za msingi Nyamoko na Itununu wakifuatilia michezo na hotoba mbalimbali kutoka kwa viongozi wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika.
Mambo yanaenda yakiongezeka kutokana na burudani na jumbe mbalimbali zilizotolewa na wanamichezo na viongozi mbalimbaliwa serikali na kisiasa.
Wanafuatilia michezo mbalimbali katika uwanja wa Nyamoko ikiwa ni katika kuhitimisha kilele cha siku ya mtoto wa Afrika.
Mkuu wa wilaya akikagua timu kabla ya kuanza michezo.
Wanafuatilia michezo mbalimbali.
Diwani viti maalum Esther Nyamhanga akiwaasa wazazi kusomesha watoto wao hasa wa kike na kuachana na vitendo vya kuwakeketa kwa kuwa madhara yake ni makubwa sana .
Michezo ilikuwa sehemu ya kufikisha ujumbe.
Wanafunzi wakiimba nyimbo mbalimbali za kuitaka jamii iepuke vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo suala la ukeketaji kwa watoto wa kike.
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Maftah Ally akikagua timu ya wasichana wa shule za Nyamoko na Itununu ikiwa ni katika kuhitimisha kilele cha siku ya Mtoto kiwilaya katika kijiji cha Nyamoko.
0 comments:
Post a Comment