WAIMBAJI WA KWAYA WAJITOSA KUPIGA
VITA MAUAJI YA WATU WENYE UALIBINISM
Ukosefu wa
elimu na hofu ya Mungu ni chanzo cha watu wengi kujihusisha na matendo ya
ukatili ikiwemo mauaji ya watu wenye Ualibism katika maeneo mengi hapa nchini.
Meneja wa
Benki ya NMB Tawi la Mugumu wilayani hapa Mkoa wa Mara William Bajunana
akiongoza watu kuchangia fedha na vitu mbalimbali kwa ajili ya watu wenye Ualibinism wakati wa Tamasha la Uimbaji kwenye
viwanja vya kanisa Katoliki Mugumu,alisema vitendo hivyo vinachafua sifa ya
taifa na mikoa ya kanda ya Ziwa.
Bajunana
ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha hilo lililoandaliwa na Mwimbaji
kutoka Kanisa la KKKT Angaza Igoma jijini Mwanza Lucy Haruni kwa ajili ya
kutafuta fedha ya kuwanunulia pikipiki watu wenye Ualibinism ili iwasaidie kupata
kipato,alisema pamoja na kuwa wilaya ya Serengeti haijawahi kukumbwa na matukio
kama hayo,lakini picha ya nchi ni mbaya kutokana na matendo hayo.
“Kila mmoja
anatakiwa kuguswa na tatizo hili ambalo limechangia wenzetu wenye ulemavu wa
ngozi kuuawa kwa misingi ya imani ya kishirikina,na hili ni tatizo kubwa la
wananchi wasiopenda kufanya kazi kupata vipato vyao badala yake wanajiingiza
kwenye mambo ambayo kimsingi hayana ukweli,tunahitaji kumhusisha Mungu zaidi
ili kuvunja nguvu ya shetani,”alisema.
Alisema
Kampeini hiyo inayofanywa na watumishi wa Mungu kwa nyimbo inatakiwa kuungwa
mkono zaidi ili watu waweze kubadilika kwa kupitia mahubiri ya kwaya,”naomba
kila mmoja alione hili kama janga maana hawa ni ndugu zetu hawakupenda kuzaliwa
hivi,”alisema.
Akizungumzia
lengo la Kampeini hiyo Lucy Haruni alisema nikupata fedha za kuwanunulia pikipiki moja watu wenye Ualibinism ili iwasaidie kuingiza
kipato kwa kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi,”kwa kuwa tatizo hili si la
dhehebu moja ndiyo maana nimeshirikisha madhehebu mengi kwa kuwa hii ni vita na
inagusa uumbaji wa Mungu,”alisema.
Katika
Tamasha hilo jumla ya zaidi y ash 2.5 milioni ikiwa ni fedha taslimu na ahadi
zilitolewa,huku Bajunana pamoja na kuchangia sh 1 mil,akiahidi kuwa kupitia
Benki ya NMB kwenye kitengo cha Jamii waombe ili waweze kusaidiwa.
Mwisho.
Paroko wa Kanisa Katoliki Mugumu Alois Magabe akifungua tamasha hilo kwa maombi
Watu wengi walishiriki katika tamasha hilo wakiwemo watoto kama inavyoonekana hapa.
0 comments:
Post a Comment