Serengeti Media Centre.
.
Mkazi mmoja
wa Kitongoji cha Nyansarari kijiji cha Masinki kata ya Magange wilayani hapa
Mkoa wa Mara Mangure Chacha(40)anashikiliwa
na Polisi kwa tuhuma za kumnajisi mtoto
wake wa miaka miwili.
Polisi
wilayani hapa ,uongozi wa kijiji na afisa mtendaji wa kata hiyo Ngeya Alfred
wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo,ambalo ni lapili kutokea katika kata hiyo ambapo Mei 25 mwaka
huu mkazi wa kijiji cha Magange Chacha
Kisamo(35)alimbaka mtoto wa miaka 13 na kumsababishia maumivu na kukamatwa
kisha kufikishwa mahakamani,hata hivyo mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana.
Afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Masinki Maitari Hunda akiongea na Serengeti Media Centre
kwa njia ya simu alisema kuwa tukio hilo
linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia 14 mwaka huu nyumbani kwa mtuhumiwa ,ambaye
kabla ya kufanya unyama huo alimpiga mke wake na kumfukuza nyumbani kwake.
“Baada ya
kupata taarifa tulifuatilia nyumbani kwa mtuhumiwa na kumkuta mtoto amelala
kitanda cha baba yake huku ameumizwa…tulipomuuliza
mtuhumiwa ambaye alionekana kulewa alidai hajui na wala hajatenda,lakini
anakiri kuwa alilala na mtoto,”alisema.
Hata hivyo Mama
mzazi wa mtoto Christina Joseph(19)alisema juni 13 majira ya saa 2 usiku mme
wake alifika akiwa amelewa na kuanza kumshambulia huku akimwapia kuwa atamuua
kwa kuwa hafanyi kazi za nyumbani kwake kama anavyotaka.
“Toka juni
11 mwaka huu ilikuwa ni kipigo tu kwangu au kwa mtoto huku akisisitiza
kuniua,na juni 13 hali ilikuwa mbaya zaidi,nikaamua kukimbia na kulala kwa mke
mdogo wa Mwenyekiti wa kijiji,mtoto wangu alikuwa amelala ndani ya nyumba ya
mama mkwe…nilipotoka akamfuata na kuja kulala naye ndipo akamfanyia ukatili
huo,”alisema na kuongeza.
“Saa 12
alfajiri nilirudi nyumbani na kumkuta mtoto amelala kitandani uchi,wakati mimi
nilimwacha akiwa amevaa,aliponiona akawa anashika sehemu za siri huku analia
,kumwangalia nikakuta ameingiliwa maana mbegu za kiume zikiwa zimetapakaa nje
na damu ikivuja,nikatoa taarifa kwa majilani kisha ofisini na kumkamata
mtuhumiwa,”alibaisha.
Hata hivyo
alimpompeleka mtoto wake zahanati ya Masinki kwa ajili ya kupata
matibabu,alikataliwa kwa madai kuwa lazima aende na fomu ya
Polisi(PF3),masharti ambayo yalimshinda kutokana na umbali,hata hivyo polisi
kupitia dawati la jinsia waliingilia kati kwa ajili ya kusimamia matibabu ya
mtoto huyo.
Alipotakiwa
kutoa ufafanuzi kuhusiana na kiini cha mgogoro huo alikiri kuwepo kwa muda
mrefu toka mwaka 2011 baada ya kumuoa akiwa mke wa pili akimdai kuwa
hazai,”baada ya mgogoro huo niliondoka na kwenda kwetu nikakaa kwa muda na
kupata mtoto,wazazi wake na wa kwangu wakaniambia nirudi ,naye akakubali
tukawatunaishi vizuri,lakini akaanza kubadilika taratibu,”alisema.
Mtoto na Mama watoroshwa kupoteza ushahidi.
Katika
Mazingira ya kutatanisha Christina akiwa na mtoto aliyenajisiwa na baba yake
ametoroshwa na ndugu wa mtuhumiwa ili kupoteza ushahidi wa tukio hilo.
“Polisi
baada ya kufika waliuliza mtuhumiwa nikawaonyesha wakaanza kumhoji,wakauliza
mama na mtoto walipo ili waweze kuchukua taarifa kabla ya kuondoka,niliwajibu
yupo kwa kuwa nilijua hayuko mbali,nikatuma mgambo wamwite,hata hivyo
hakupatikana na kuibua wasiwasi kwa wananchi,”alisema Mtendaji wa kijiji.
Hata hivyo
aliambiwa na wananchi kuwa mama huyo ameonekana akipanda boda boda akiwa na
mwanae na shemeji yake ambaye ni mdogo wa
mtuhumiwa wakaelekea Sirori Simba,hali iliyowalazimu kufuatilia kwa
gari.
“Tulifanikiwa
kumpata bodaboda aliyewabeba akasema kuwa alikodiwa kuwapeleka hadi Sirori Simba
na kuwaacha hapo ambapo walionekana kukodi pikipiki kuelekea Buhemba wilaya ya
Butiama,kwa ujumla tukio hilo limeacha maswali mengi lilivyotokea maana
kutoroshwa kwa mama na mtoto wamepoteza ushahidi,”alisema.
Alipoulizwa
mikakati iliyokuwa inaendelea kabla ya kutoroshwa kwa mama na mtoto,alidai kuwa
ndugu walikuwa wakizunguka ofisini hapo wakionyesha wazi kujadiliana na mama wa
mtoto kila wakati,na inadaiwa kuna kaka yake na mtuhumiwa aliyeko Bunda ndiye
anadaiwa kuratibu zoezi zima la kuwatoroshwa baada ya kutuma fedha kwa ndugu
zake kijijini hapo.
Mkuu wa
wilaya Maftah Ally alisema mtuhumiwa bado anashikiliwa na polisi na kuhusu mama
na mtoto wake wanaendelea kusakwa ikiwemo na wale waliohusika kuwatorosha.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment