Mapokezi ya vifaa yalishirikisha viongozi wa kada mbalimbali.
WADAU WAAMUA KUJENGA BWENI KUNUSURU
WASICHANA NA MIMBA,
Serengeti Media Centre.
Ili
kuwanusuru wanafunzi wa shule za sekondari na mimba,utoro na ndoa za utotoni
zinazoendelea wilayani hapa Mkoa wa Mara shirika lisilo la kiserikali la Girls Education Support Initiatives(gesi)limeanza
kujenga bweni la wasichana katika
sekondari ya Ring’wani.
Inadaiwa
wasichana zaidi ya 36 wamekatishwa masomo wa sekondari na shule za msingi wilayani
hapa wamekatishwa masomo kutokana na ujauzito,pia ndoa za utotoni na utoro huku
ukosefu wa mabweni ukitajwa kama chanzo cha tatizo.
Katibu
Mtendaji wa shirika hilo lenye makao makuu yake wilayani hapa Catherine Ruge
alisema wameanza ujenzi wa bweni litakalosaidia watoto wa kike 56 ambao
wamepanga kijijini hapo katika mazingira yanayochangia kukata tamaa ya kusoma.
“Watoto
wamepanga kijijini hali inayowafanya waishi maisha kama ya unyumba,wengine
wanatoka mbali kiasi kwamba hawahudhurii masomo kwa wakati,waanza wengi
wanamaliza wachache na hawafanyi vizuri,ndiyo maana tukatafuta watu wa
kutusaidia ili kuwanusuru watoto wa kike,”alisema.
Mwalimu Mkuu
wa shule hiyo Elibariki Mwita alisema shule hiyo inahudumia kata mbili za
Ring’wani na Magange na wengi wanatoka mbali ,wanalazimika kupanga mtaani na
wengine wanatembea umbali mrefu hali ambayo inawafanya waache masomo.
“Kwa kipindi
cha miaka 13 wasichana 3 pekee ndiyo waliofaulu kwenda kidato cha tano,mwaka
2013 tulipokea wasichana 37 kuanza kidato cha kwanza,lakini waliopo sasa ni 20
pekee ,wasichana 9 wameacha shule ,wawili
wamerudia kidato cha pili na uhamisho wasichana watano,ukosefu wa bweni ni
tatizo kubwa hapa kwa kuwa maisha ya mtaani huwageuza kuwa wake za
watu,”alisema.
Na kuwa
katika mitihani ya majaribio ikiwemo ya BRN wasichana wote hakuna aliyefaulu
chanzo kikiwa ni ukosefu wa mabweni.
Ruge
akizungumzia mkakati wao alisema ujenzi huo wanategemea kukamilika mwishoni mwa
mwaka huu,”inagharimu zaidi y ash 85 milioni kama hakuna nguvu za
wananchi,lakini kwa kushirikisha wananchi ambao wamekubali kuchangia nguvu kazi
tunategemea kazi hiyo itagharimu zaidi y ash 50 milioni,”alisema.
Alisema
shirika lao linalolenga kumsaidia mtoto wa kike wilayani humo lina malengo ya
kusaidia shule mbalimbali kadri wanavyopata msaada,aliomba wadau wengine
kuwekeza kwenye elimu kama njia pekee ya kumkomboa mtoto wa kike anayekabiliwa
na vikwazo vingi ikiwemo mila na desturi.
Diwani wa
kata ya Magange George Mahemba alisema kupitia msaada huo wananchi wamekubali
kuchangia ili kuwanusuru watoto wa kike .
Mwisho.
Catherine akiwa na wazazi na baadhi ya viongozi wa kijiji na kata ya Ring'wani na Magange baada ya mtoto wa kike kujitokeza kuwasaidia wadogo zake ili waweze kupata mazingira mazuri ya kuishi na wasome.
0 comments:
Post a Comment