Fahari ya Serengeti

Friday, June 17, 2016

SERIKALI,VIONGOZI WA DINI NA WADAU MBALIMBALI WAUNGANISHA NGUVU KWA AJILI YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.

Viongozi wa madhehebu  na wawezeshaji wa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti wakiwa kwenye Picha ya Pamoja baada ya mafunzo juu ya Ukatili wa Kijinsia ikiwemo suala la Ukeketaji ,miongoni mwa mikakati ya Mradi huo ni kufikia makundi yote kwa lengo la kushirikiana katika vita ya kutokomeza ukeketaji wilayani humo.
Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa kwenye mjadala kwenye vikundi vyao ,na kuweka mikakati mbalimbali ya kupambana na ukatili wa kijinsia wilayani humo.
Mikakati ikiendelea kuwekwa.
Mwezeshaji wa mada ya ushauri wa kisaikolojia Jane Mwakalila akiandaa nondo kwa ajili ya kuwapa viongozi wa dini,mada ambayo inawasaidia viongozi hao kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto wanaoathiriwa na mfumo huo,baadhi ya wazazi ,ngariba na wazee wa mila.
William Mtwazi mwanasheria kutoka Lhrc ambaye ni Afisa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti akiwa anaandaa mambo ya msingi ya kuwasilisha kwa viongozi wa madhehebu .
Majadiliano ya kwenye vikundi
Uwasilishaji wa kazi za vikundi inaendelea chini ya mwezeshaji wa somo la Ushauri wa Kisaikolojia Jane.
Mchungaji Nuhu wa Jeshi la Wokovu akiwasilisha kazi ya kikundi chake.
Wanafuatilia mjadala kuhusiana na mada ya ushauri wa kisaikolojia  ambayo itawawesha viongozi wa dini kujua mbinu za kuwasaidia watu wanaokuwa wamepata matatizo ya ukatili wa kijinsia.
Kuna wakati walishapa kutokana na jinsi mada zilivyokuwa zikitolewa.

Ustaadhi Mikidadi Iddy akiwasilisha kazi ya kikundi chao.
Anasisitiza jambo kwa uzito wake mwezeshaji kama inavyoonekana.
Maneno yamewaingia sawasawa kama inavyoonekana lazima mkakati ukasimamiwe ili kuwanusuru watoto wa kike na ukatili wa kijinsia.
Burudani mbalimbali zinatolewa kama hivyo.
Mmabo yanaenda kama yakiongezeka,

0 comments:

Post a Comment