Fahari ya Serengeti

Sunday, January 21, 2018

WAZIRI MKUU AMALIZA ZIARA YA SIKU 7 MARA NA KUACHA MAAGIZO MAZITO

 Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amehitimisha ziara ya siku saba Mkoani Mara na kuacha maagizo mazito kwa viongozi ikiwemo kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa Musawa Saidi Gantala na kuitaka Takukuru kuendelea na uchunguzi wa miradi yote ya Maji baada ya kubainika kutafunwa kwa fedha za miradi hiyo.

Amemwagiza Naibu Waziri Tamisemi na Katibu Mkuu wizara ya Maji na Umwagiliaji kubaki mkoani humo wakifuatilia kwa kina taarifa za Miradi ya Maji kwa kukutana na wahandisi wote wa Maji mkoa huo na kumpa taarifa hivi karibuni.

Amewaagiza viongozi na watendaji kutatua kero za wananchi na wasikae ofisini kwa kuwa kupokelewa kwa mabango kila alikokwenda ni ishara mbaya kiutendaji.

 Viongozi mbalimbali wakifuatilia maelekezo ya Waziri Mkuu katika Ukumbi wa Uwekezaji Musoma




Sunday, January 14, 2018

SIKU CHACHE BAADA YA MFUNGWA KUKAMATWA KWA UJANGILI WAGENI WASIOJULIKANA KUTIMULIWA ROBANDA

 Wakazi wa kijiji cha Robanda wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wametoa siku mbili kwa wageni wote wasiojulikana kijijini hapo kuondoka kabla ya kuanzishwa msako mkali,uamzi huo umefikiwa kwenye kikao cha jamii(ritongo)ambapo wamelaani mauaji ya tembo yaliyofanywa na majangili wakishirikiana na mfungwa mkazi wa Kibiti.
Pia wamepiga marufuku watuhumiwa wa ujangili Hamisi Gamaho na Nyamincha kurudi kijijini hapo,pia ndugu zao wameonyeshwa njia ya kutokea kwa kuwa wamekuwa sehemu ya ujangili huo kwa kutokusema ama kukemea vitendo vya ujangili na kuingiza silaha kijijini.
 Kwa pamoja wanasisitiza watuhumiwa wakiachiwa wakikanyaga kijijini watachukua maamzi magumu.
 Mama yake na Hamisi Gamaho mmoja wa watuhumiwa wa ujangili akiwa amewekwa kiti moto na wananchi ambapo wamemtaka kuwapisha kijijini hapo warudi Nyichoka kwa kuwa vitendo vya kijana wake vimedhalilisha jamii nzima ya Robanda.

 Msisitizo ulitolewa


Saturday, January 13, 2018

WANACCM WATAKIWA KUJITOKEZA KAMPEINI YA JENGA HOSPITALI KWA SH 1000

 DC Serengeti Nurdin Babu akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha januari -desemba 2017 katika kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya,pamoja na mambo mengine amewasisitiza wanaCcm kuwa mstari wa Mbele kuchangia kampeini ya Jenga Hospitali ya Wilaya kwa sh 1000 ili waweze kupata fedha za kukamilisha ujenzi awamu ya kwanza na kuruhusu kufunguliwa mwezi februari mwaka huu.
 Wanafuatilia
 Wanafuatilia taarifa
 Anasisitiza

WANNE WAJIEUNGUA CHADEMA NA KUJIUNGA NA CCM SERENGETI

 Mmoja wa wanachama wa Chadema kutoka Mtaa wa MCU Mugumu wilaya ya Serengeti akionyesha kadi ya Chadema muda mfupi baada ya kujiengua na kupokelewa na CCM wakati wa Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya.
 Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Serengeti wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao cha kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha januari hadi desemba 2017.

 Dc Serengeti Nurdin Babu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM MWAKA 2017
Wanachama waliojieungua Chadema na kujiunga na CCM.

Monday, January 8, 2018

UJENZI WA KANISA LA MT FRANSISKO WA ASIZI MUGUMU INAENDELEA VIZURI

 Ujenzi wa kanisa Katoliki Parokia ya  Mt Fransisko wa Asizi Mugumu Serengeti kwa michango ya waumini na wadau mbalimbali walio ndani na nje ya wilaya ya Serengeti inaendelea vizuri kama inavyoonekana,waumini na wadau wa maendeleo mnaombwa kuendelea kuchangia kazi hii,maana ni HERI KUTOA KULIKO KUPOKEA...
 Kazi inaendelea


MBUNGE ATOA MSAADA KWA WATOTO WA MAZINGIRA MAGUMU

 Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mara Catherine Ruge(Chadema)ametoa msaada wa sare kwa wanafunzi 100 katika shule  tano za msingi  ikiwemo Majimoto,Ring'wani,Magange,Remng'orori ambao wanaishi katika mazingira magumu,lengo ni kufikia watoto zaidi ya 400 wilayani  Serengeti,msaada huo unalenga kuliwezesha kundi hilo kusoma .
Anatimiza dini iliyo ya kweli kwa kuwahudumia wahitaji,hapo anamsikiliza mmoja wa watoto walionufaika na msaada huo.
Add caption

 Mbunge anasikiliza shida mbalimbali za watoto wa shule ya msingi Majimoto

 Anahimiza umuhimu wa kusoma mara alipokutana na wanafunzi wa sekondari ya Ring'wani

Picha ya pamoja na viongozi ilipigwa

WAZAZI WAJITOKEZA KUPELEKA WATOTO KUANZA MASOMO MUGUMU SERENGETI

 Baadhi ya wazazi wa Mjini Mugumu wilaya ya Serengeti wakiandikisha kwa mwalimu Nyamatage Musagasa wa shule ya Msingi Mugumu A wilayani Serengeti,ikiwa ni siku ya kwanza kuanza masomo mwaka huu.
 Elimu ndiyo msingi wa maisha
 Watoto nao wako tayari kwa kuanza masomo kama wanavyooonekana
Kila mzazi na mwanae ili ahakikishe anasajiriwa kwa ajili ya kuanza masomo

MFUNGWA ANASWA KWA UJANGILI WA TEMBO SERENGETI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Jafari Mohamed akiangalia moja ya bunduki zilizokamatwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambazo zilikuwa zikitumiwa na majangili walioongozwa na Mfungwa Khamisi  Mussa Bweha kutoa Kibiti Rufiji ambaye alifungwa miaka mitatu mwaka jana kwa kosa la kukamatwa na silaha kinyume cha sheria Mwanza ,Hata hivyo amekamatwa kwa tuhuma za kuua tembo wawili katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti akishirikiana na wenzake watatu wakazi wa wilaya ya Serengeti.
Katika tukio hilo Polisi walifanikiwa kupata bunduki mbili Riffle 458 risasi zake tano katika kijiji cha Robanda na bunduki AK-47 na risasi zake 130 iliyokuwa imefukiwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
 wanaangalia vitu vilivyokamatwa


 Mzigo wa risasi ulionaswa