Fahari ya Serengeti

Tuesday, October 17, 2017

NG'OMBE 1179PARK NYIGOTI WATAIFISHWA NA MAHAKAMA

NG’OMBE 119,MBUZI 20 KUPIGWA MNADA HUKU WAMILIKI WAKIKWEPA KIFUNGO KWA KULIPA FAINI,
Na Serengeti Media Centre
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya SerengetI Mkoa Mara imetaifisha ng’ombe 119 na mbuzi 20 huku washitakiwa wawili wakazi wa kijiji cha Park nyigoti wakilazimika kulipa faini ya sh 800,000 kukwepa kifungo cha miaka mitatu jela.
Katika kesi ya Jinai namba 219/2017  Hakimu wa Mahakama hiyo Ismael Ngaile amemhukumu Ntagiri Manyeresa(44)mkazi wa kijiji cha Park nyigoti baada ya kutiwa  hatiani kwa makosa matatu aliyoshitakiwa nayo.
Akitoa adhabu  hiyo hakimu Ngaile amesema kwa kosa la kwanza mshitakiwa anatakiwa kulipa faini ya sh 200,000 au kifungo cha mwaka mmoja jela, kosa la pili anatakiwa kulipa faini sh 300,000 au jela miaka mitatu na kosa la tatu kulipa sh 300,000 au kifungo cha miaka mitatu.
Ambapo kama atashindwa kulipa faini atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kama atalipa faini atalazimika kulipa sh 800,000 ,hata hivyo amelipa na kuachiwa huru.
Hakimu Ngaile amesema ng’ombe 100  waliokamatwa ndani ya Pori la Akiba la Ikorongo watataifishwa chini ya kifungu cha 111(1)(a)(3)na (4) cha Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 ikisomwa pamoja na kifungu namba 351 (1)(2)na(4)cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura namba 20 ya mwaka 2012.
Katika Utetezi Mshitakiwa ameomba Mahakama imhurumie kwa kuwa umri wake ni mkubwa ,ana mke, watoto na anategemewa na mama yake,hata hivyo upande wa waendesha mashitaka umeomba adhabu kali itolewe ili liwe fundisho kwa watu wengine.
Wakati huo huo Katika kesi ya Jinai namba 220/2017 katika Mahakama hiyo hiyo mshitakiwa Nelson Museti Mwera(31)mkazi wa kijiji cha Parknyigoti amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya sh 800,000 .
Amesema  ng’ombe 19 na mbuzi 20  watataifishwa na serikali chini ya kifungu cha 111(1)(a)(3)na (4) cha Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 ikisomwa pamoja na kifungu namba 351 (1)(2)na(4)cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura namba 20 ya mwaka 2012.
Mapema waendesha Mashitaka Shukrani Msuya wa Senapa na koplo wa Polisi Renatus Zakeo mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo Ismael Ngaile  wameikumbusha mahakama kuwa katika kesi ya jinai namba 219/2017,Manyeresa  septemba 31,2017 saa 5 asubuhi alikamatwa eneo la Mto Manchira ndani ya Pori la Akiba la Ikorongo.
Na kuwa oktoba 4,2017 alifikishwa mahakamani kwa makosa matatu ya kuingia ndani ya Pori la Akiba bila Kibali kinyume cha Kifungu cha Sheria 15(1)(2) cha Sheria Namba 5 ya Wanyamapori ya Mwaka 2009.
Kosa la pili ni kuchunga mifugo katika Pori la Akiba kinyume na kifungu cha 18(2)(4)cha Sheria Namba 5 ya wanyamapori ya mwaka 2009,na kosa la tatu ni kuharibu uoto wa asili katika Pori la Akiba la Ikorongo kinyume na kifungu cha 18(1)(3)cha Sheria ya Wanyapori namba 5 ya mwaka 2009,ambapo alikutwa na ng’ombe 100.
Katika kesi ya jinai namba 220/2017  wameiambia Mahakama kuwa  31,2017  mshitakiwa Nelson Museti Mwera alikamatwa katika eneo la Burumbaga ndani ya Pori la Akiba la Ikorongo na kufikishwa mahakamani kwa makosa matatu ya kuingia,kuchungia ndani ya eneo hilo kinyume cha sheria na kuharibu uoto wa asili.
Mwisho.


Saturday, October 14, 2017

DC AWAMWAGIA SIFA WAANDAJI WA KONGAMANO

 DC Serengeti Nurdin Babu amewamwagia sifa waandaji wa kongamano la miaka 18 bila Mwalimu Nyerere ambao ni Serengeti Media Centre,Frankfurt Zoological Society,na Chuo cha Utalii Serengeti,kuwa ni kwa mara ya kwanza toka mwalimu Nyerere aage dunia
 watoa mada wakijibu maswali na kupokea michango ya washiriki

Baadhi ya washiriki

BURUDANI KUTOKA KIKUNDI CHA COCOBA BONCHUGU KILIHANIKIZA KUMBUKUMBU YA MIAKA 18 YA NYERERE SERENGETI

Wasanii kutoka kikundi cha COCOBA Bonchugu wilaya ya Serengeti wakiburudisha washiriki wa kongamano la miaka 18 bila Mwalimu Nyerere ukumbi wa Kanisa Katoliki Mugumu


KATIKA KUMUENZI MWL NYERERE JAMII YATAKIWA KUACHA UJANGILI

 Dc Serengeti  Nurdin Babu wa tatu kutoka kulia akipitia taarifa kabla ya kufungua Kongamano la Wadau wa uhifadhi na Utalii katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki  Mugumu,amewataka wananchi kuwafichua watu wanaojihusisha na ujangili kwa kuwa unaathiri Maliasili na pato la Taifa.
Amesema katika kumuenzi hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa mhifadhi mkuu kila mmoja anatakiwa kuwa mlinzi wa Maliasili zetu.
Kongamano hilo ambalo limeshirikisha wadau wa wa uhifadhi kutoka wilaya za Serengeti ,Meatu na Waandishi wa habari limeandaliwa na Serengeti Media Centre,Frankfurt Zoological na Setco kwa ufadhili wa EU,GRUMET FUND NA SENAPA.
 Washiriki wa mdahalo kutoka taasisi mbalimbali wakifuatilia mijadala
 Wanafuatilia mjadala

Masegeri Tumbuyo toka Frankfurt kwa niabaya waandaji akitoa lengo la kongamano hilo

Thursday, October 12, 2017

WAZEE WA MILA WAZIDI KUWAONYESHEA KIDOLE WATAKAOKEKETA WATOTO

 Wakati ikiadhimisha siku ya mtoto wa Kike na kukemea wanaume wakwale,wazee wa mila wa koo ya Inchugu nao wanazidi kuchanja mbuga maeneo mbalimbali kuwakemea wazazi watakaokeketa watoto wa kike kukiona
 Wanawekeana masharti ,wazee watakaokiuka wenzao kuadhibiwa
 Wanapeana tisheti zenye ujumbe wa kupinga ukeketaji
 Fundi Mitambo akiwa kazini
Anahangaika na mambo yake

RADI YAUA NG'OMBE 4 NA KONDOO 8 SERENGETI

 Wakazi wa Kitongoji cha Ramakendo kata ya Morotonga wilaya ya Serengeti wakiangalia mzoga wa ng'ombe kati ya waliopigwa radi iliyoambatana na Mvua,hata hivyo afisa mifugo ameamru mizoga hiyo kuzikwa,uamzi ambao umepingwa na wananchi waliokuwa wamejiandaa kuwachuna ili wagawane nyama.

 Wanatafakari uamzi wa afisa mifugo wa kata ya Morotonga kuwataka wafukie mizoga wakati wao wamejiandaa kwa kugawana kitoweo
 Tafakari inaendelea

 Kila mmoja anasikitikia tukio hilo



ILIVYOKUWA SIKU YA MTOTO WA KIKE SERENGETI

 Mkurugenzi wa shirika la GESI ambaye ni Mbunge Viti Maalum (Chadema)mkoa wa Mara Catherine Ruge akisisitiza jamii kuwafichua watu wanaochangia kuharibu maisha ya watoto wa kike na wasifikie ndoto zao
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja
 Maandamano kuelekea Uwanja wa Mbuzi
 wanafuatilia


 Viongozi wanapitia taarifa mbalimbali
 maigizo yalikuwa sehemu ya burudani

 Anafuatilia maigizo




Wednesday, October 11, 2017

KONGAMANO LA MIAKA 18 BILA MWL NYERERE KUKUTANISHA WADAU WA UHIFADHI SERENGETI

fRANKFURT ZOLOGICAL SOCIETY(FZS)SERENGETI TOURISM COLLEGE(SETCO)NA SERENGETI MEDIA CENTRE(SMC)wameandaa KONGAMANO LA MIAKA 18 BILA MWL NYERERE,JE TUNAMUENZIJE KATIKA ULINZI WA MALIASILI ZETU?,Washiriki watatoka ndani na nje ya Mkoa wa Mara ,SENAPA,TAWIRI,IKONA WMA,FRANKFURT ,GRUMETI FUND/RESERVES NA IKORONGO (IGGR)watatoa mada,kwa walioalikwa hili si la kukosa .

Tuesday, October 10, 2017

CHANGAMOTO ZA ELIMU ZAIBULIWA

 Wanafunzi wa shule za Msingi za Kata za Mugumu na Stendi Mpya Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu,ambapo changamoto za elimu zimeibuliwa ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa ,walimu na wanafunzi kutokupata chakula cha mchana wawapo shuleni.
Hata hivyo jamii imetakiwa kushirikiana na wataalam kutatua changamoto hizo ikiwemo kuchangia chakula shuleni ili kuwawezesha watoto kushiriki vizuri masomo yao.
 Burudani mbalimbali zikiendelea
 Wanawasilisha ujumbe
 Dc akipata taarifa mmbalimbali za kukabiliana na changamoto za elimu

Wjasiriamali wameitumia fursa hiyo kupata kipato

WALIMU WATAKIWA KUHAKIKISHA TATIZO LA KUTOKUJUA KUSOMA NA KUANDIKA LINAKWSHA

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Nurdin Babu akipata maelezo kutoka kwa walimu jinsi wanavyotumia mbinu mbalimbali kuhakikisha watoto wanajua kusoma,kuandika na kuhesabu wakati wa kuhitimisha wiki ya elimu wilayani hapo,Hata hivyo amewaagiza kuhakikisha tatizo la wasiojua kusoma na kuandika linakwisha wilayani hapo.
 Mikakati mbalimbali inafafanuliwa na walimu
 Mbinu nyingine ni kutumia michezo
Hongera sana mtoto kwa kufanya vizuri