Fahari ya Serengeti

Monday, August 21, 2017

NEMBO YA TAIFA KIVUTIO KIKUBWA KWA WATALII

 Twiga ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti akiwa ametulia

 Pundamilia ni miongoni mwa wanyama wanaovutia ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti

FIKA KITUO CHA UTALII HIFADHI YA SENAPA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI

 Kituo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kimejaa taarifa mbalimbali na wanyama na vitu vya kale kama mafuvu ya wanyama mbalimbali,mafuvu hayo yenye historia ya miaka dahari,kumbukumbu hizo ni muhimu sana kuonyesha historia za uhifadhi na utalii.

WATALII WA NDANI NA WA NJE WAOMBA WANANCHI KUTEMBELEA VIVUTIO

 Baadhi ya watalii wa kutoka nchini Denmark wakiwa katika picha ya pamoja na watalii wa ndani kutoka The Sa Shine English Medium Nursery School Mugumu baada ya kukutana ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kusisitiza wananchi kujitokeza kutembelea vivuto vya utalii.
Wamesema watanzania hawatakiwi kusoma ama kuangalia vivutio kwenye vyombo vya habari bali wafike ikiwa ni njia pekee ya kukuza pato la taifa.
 Watalii wa ndani na wa nje wakijadiliana mambo mbalimbali.
 Tumetokelezeaaa
 Watalii kutoka Denmark baada ya kuvutiwa na watoto hao wadogo kuanza kufanya utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wameamua kuwatunuku zawadi mbalimbali.


Watoto wamepata vitabu ikiwa ni kukuza maarifa ya kujua masuala mbalimbali ya dunia,hakika utalii wa ndani huanza na watoto wadogo.

Sunday, August 13, 2017

MAPESA CUP,MAGETA FC IMEFANYA YAKE YAISAMBARATISHA KIBEYO FC

 Baadhi ya mashabiki wa mpira wa Miguu  wasiokuwa na kiingilio cha sh 300 wakifuatilia mchezo kati ya Mageta Fc na Kibeyo Fc katika Uwanja wa Sokoine Mjini Mugumu wilaya ya Serengeti katika Ligi ya Mapesa Cup ,katika mchezo huo Mageta Fc imeisambaratisha vibaya Kibeyo Fc kwa mabao 4-2
 Wanafuatilia mchezo
 Wachezaji wa Mageta Fc wakishangilia bao la tatu
 Kila mmoja anataka kushuhudia mpambano huo kwa kwa mbinu mbalimbali
Mambo yanazidi kuongezeka

Friday, August 11, 2017

MAPESA CUP,ITUNUNU FC KUUMANA NA SUPER EAGLES UWANJA WA SOKOINE MUGUMU


Timu ya Itununu Fc inamentana na Super Eagles leo Uwanja wa Sokoine Mjini Mugumu wilaya ya Serengeti kuwania kombe la Mapesa,katika mchezo wa jana timu za Miseke na Muungano zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 ,ligi hiyo inayoshirikisha timu 14 imeandaliwa na walimu na mshindi wa kwanza atapata ng'ombe wawili,mshindi wa pili ng'ombe mmoja na mshindi wa tatu mbuzi wawili,pia zawadi mbalimbali zitatolewa kwa mfungaji bora,kipa bora ,mchezaji bora na waamzi wa ligi hiyo,kumbuka kiingilio ni sh 300 kwa kila mtu,wahi nafasi kwa kuwa jukwaa huu linajaa haraka.






Thursday, August 10, 2017

JUMA PORINI CUP YAWALETA PAMOJA WAKAZI WA NATTA SERENGETI


Diwani wa Kata ya Natta wilaya ya Serengeti ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Juma Porini mwenye shati la draft akiwa na viongozi na wachezaji wa timu mbalimbali za mpira wakati wa Kombe la Porini Cup ,
Mashindano hayo ambayo yameshirikisha timu 12 za mpira wa miguu ,mbio za magunia,kufukuza kuku,mbio za baiskeli ,mbio ndefu na netibali na kufuatiwa na utoaji wa zawadi za zaidi ya sh 8 mil kwa washindi wote ikiwemo wachezaji ,waamzi na kamati ya maandalizi.
Aidha katika mashindano hayo wamefanikiwa kuunda timu ya mpira wa miguu kata ya Natta ambayo amesema atakuwa mlezi wake.

Nahodha wa timu ya netiboli ya Natta Sekondari wilaya ya Serengeti Jakline akipokea kombe kutoka kwa mgeni rasmi kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Wambura Sunday baada ya kuibamiza timu ya Grumeti kwa mabao 13-4 na kuibuka bingwa Juma Porini Cup.
 Wachezaji wa timu ya Grumeti Fc wakiwa katika picha ya pamoja.
 Mgeni Rasmi Wambura Sunday akikagua timu ya netiboli ya Grumeti kabla ya kupokea kichapo kutoka kwa vijana wa  Natta sekondari kwa  magoli 13-4
 Burudani mbalimbali zilihanikiza katika kwenye mashindano ya Porini Cup
 Mmabo yanaenda yakiongezeka,watu wa rika mbalimbali wameshiriki
 Mwali aking'ara akisubiri mlengwa
 Porini Cup imewaleta pamoja watu mbalimbali,hapo ni jaza ujazwe wanapigwa picha na kupiga picha,
 Zawadi zikitolewa

 Kila mtu anavuna alichopanda zawadi zinazidi kumiminika


 Washabiki walikuwa lukuki




Zawadi zawadi ni jaza ujazwe bandika bandua

Wednesday, August 9, 2017

MAPESA CUP WAHENGA MUGUMU STAR YAWABANA RWAMCHANGA FC

 Timu ya Mugumu Star (Wahenga) imeanza ligi ya Mapesa Cup kwa kuwabana vijana machachari wa Rwamchanga Fc na kulazimisha sare ya kutofungana na kugawana pointi moja moja kwenye Uwanja wa Sokoine Wilaya ya Serengeti.
Ligi hiyo ya Mapesa Cup itashirikisha timu 14  kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo inatarajiwa kukamilika septemba 13 mwaka huu,ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na ng'ombe wawili,mshindi wa pili ng'ombe mmoja na mshindi wa tatu mbuzi wawili.
Pia kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa ajili ya kipa bora,mfungaji bora na waamzi.
Kwa mjibu wa Emmanuel Mapesa mdhamini wa ligi hiyo alisema kwa kushirikiana na walimu wenzake wameanzisha ligi hiyo kwa lengo la kuibua vipaji na kuwapa uzoefu waamzi waliomaliza mafunzo hivi karibuni.
 Mugumu Star (wakongwe) wenye sare za bluu wakionyeshana ubabe na vijana wa Rwamchanga Fc uwanja wa Sokoine katika kuwania kombe la Mapesa.

WAJITOKEZA MASHINDANO YA MBIO ZA BAISKELI BONANZA LA JUMAPORINI

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Wambura Sunday akizindua mashindano ya Mbio za Baiskeli kata ya Natta ambayo yameandaliwa na diwani wa Kata hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini .

Amesema kupitia michezo mbalimbali watu wanaweza kuonyesha vipaji vyao,na kuwa uamzi wa diwani wa kata hiyo kuandaa michezo mbalimbali kunatoa fursa kwa watu kuonyesha vipaji vyao na pia kujenga mahusiano mazuri.
 Baadhi ya washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli wakiwa wanajiandaa kuanza mbio za kilometa tatu.

BONANZA LA JUMAPORINI NATTA SERENGETI LAWAPAGAWISHA WANANCHI

 Diwani wa Kata ya Natta wilaya ya Serengeti Juma Porini akiongea na wakazi wa Kata hiyo kwenye Bonanza la nane nane lililofanyika uwanja wa Natta Mbisso ,ambapo michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu,Netboli,mbio za baiskeli,kukimbia na magunia na kufukuza kuku huku wakihanikizwa na vikundi vya ngoma za utamaduni wa makabila ya Wakurya na Watatoga.
 Ngoma ya kikurya ikitumbuiza kwenye bonanza la Juma Porini
 Mashindano ya kufukuza kuku yalinogesha burudani
 Wachezaji wa timu ya Natta netbali

Natta Oyeee anasikika anasema Juma Porini

Saturday, August 5, 2017

POLISI FC BINGWA WILAYA YA SERENGETI

 Wachezaji wa Timu ya Polisi wilaya ya Serengeti wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya kuchukua ubingwa wa wilaya hiyo .

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akikagua timu ya mpira ya Kibeyo Fc kabla ya kupambana na timu ya timu ya Polisi Fc,hata hivyo timu hiyo iligomea mchezo baada ya kufungwa goli moja na kuifanya timu ya Polisi kutawazwa mabingwa wa wilaya
 Diwani wa Kata ya Kisangura Smason Wambura akimkabidhi zawadi diwani wa kata ya Nyansurura Francis Garatwa akiwakilisha timu ya Nynsurura Fc
 Nahodha wa timu ya Polisi  Fc Samwel Manyero akipokea zawadia  kutoka kwa mgeni rasmi kufuatia timu yake kuibuka mabingwa