Gari la Halmashauri ya wilaya ya Serengeti likisukumwa baada ya kukwama ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wanatoka kusindikiza Mwenge wa Uhuru eneo la Krensi kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha,hata hivyo safari iliendelea kama kawaida baada ya kulikwamua.
Monday, September 4, 2017
Sunday, September 3, 2017
MIKAKATI YA TANZANIA YA VIWANDA SERENGETI YAMVUTIA RC
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa akiwa na viongozi wa wilaya ya Serengeti kwenye eneo la ujenzi wa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti chini ya Kampuni ya Lumuye Leopard Co.Ltd eneo la Tambisa Mugumu Serengeti.
Katika mjadala wa Pamoja viongozi hao wamekubaliana kuwa huduma ya Maji na Umeme ifikishwe eneo hilo ili kurahisisha kazi za ujenzi ambao unatarajiwa kuanza wakati wowote.
Hata hivyo Ded Serengeti Juma Hamsini amemtaka mwekezaji huyo kuchangia gharama za kusambaza maji ili kuharakisha huduma hiyo,kwa kuwa katika bajeti ya Muguwasa hawakuwa na fedha za kupeleka maji eneo hilo zaidi ya kilometa mbili
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mgiye Chacha amesema yuko tayari kuchangia gharama ili kumpunguzia gharama za kufuata maji kisimani
Viongozi wakijadiliana
Rc Mlingwa amesema kazi ya serikali ni kuandaa mazingira wezeshi kwa wawekezaji,hivyo kupeleka maji na umeme ndiyo kazi ya serikali,na kuomba utekelezaji ufanyike kwa haraka.
Mgiye Chacha Mkurugenzi wa Lumuye Leopard Co.Ltd kushoto anasema kutokuwa na maji na umeme wanatumia gharama kubwa na kazi za ufyatuaji matofali inakwenda taratibu.

Saturday, September 2, 2017
BURUDANI ZILITAWALA MAKABIDHIANO YA MWENGE WA UHURU MARA NA ARUSHA
Burudani mbalimbali zilitawala makabidhiano ya mwenge wa Uhuru katika eneo la Krensi Loliondo wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha ,
Ngoma ya Masai ambayo wachezaji hurika na kutua pale pale hawasongi mbele wala kurudi nyuma
Mwenge ukikatiza maeneo ya hifadhi,raha ya utalii hiyo
Mbwembwe na madoido toka kwa wasanii mbalimbali zilihanikiza
Viongozi wa Mkoa wa Mara wakiwa wamejipanga tayari kwa makabidhiano

NG'OMBE ZAIDI YA 385542 KUWEKEWA ALAMA SERENGETI
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akizindua zoezi la uwekaji alama kwa mifugo katika kijiji cha Singisi kata ya Nagusi,amesema wafugaji wataoshindwa kuwekea alama mifugo yao,kusajiri na kuwa na vitambulisho watakuwa wamepoteza sifa za kuwa wafugaji.
Amesema mpango huo unaochangiwa na mfugaji kwa kila ng'ombe sh 500 unalenga kupunguza migogoro kati ya wafugaji ,wahifadhi,wakulima na wawekezaji kwa kuwa utaiwezesha serikali kupata taarifa sahihi za wafugaji na malisho yaliyopo.
Diwani wakata ya Nagusi Jaksoni Manyeresa akiweka alama ng'ombe
Afisa mifugo Mesanga naye akiweka alama
Wananchi wakiwa wanafuatilia maagizo ya serikali ya uwekaji alama
Wafugaji wanafuatilia kwa makini ili waweze kuanza utekelezaji bila migongano na serikali
Mjadala

Friday, September 1, 2017
MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA,WAJAWAZITO WAPEWA VYANDARUA
Ili kuttekeleza moja ya Ujumbe wa Mwenge mwaka huu,kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Amour Hamad Amour amegawa vyandarua kwa wajawazito katika zahanati ya Busawe wilaya ya Serengeti muda mfupi baada ya kuifungua kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakazi wa kata hiyo na maeneo ya jilani.
Hata hivyo mkakati ni kukifanya kituo cha afya muda si mrefu.
Itifaki ikiwa imezingatiwa
BURUDANI ZILITAWALA MKESHA WA MWENGE SERENGETI
Nuru sanaa walikuwa miongoni mwa vikundi vilivyokonga nyoyo za wananchi kutokana na burudani kem kem katika mkesha wa Mwenge Uwanja wa Mbuzi,licha ya kuwepo mvua iliyoambatana na upepo lakini wananchi hawakukimbia ,
Kupandwa kwa mti wa maadili Ikorongo sekondari ni moja ya tukio kubwa lililofanywa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa
Bweni la watoto wenye ulemavu shule ya msingi Mugumu limefunguliwa
Mkuu wa wilaya Nurdin Babu akipokea mwenge wakati wa risala ya utii ikisomwa
Wanasubiri maelekezo
Matukio mbalimbali yalijiri
Ngoma hii ilikuwa miongoni mwa zilizowaburudisha wananchi
Kiongozi wa Mbio za mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour akitoa salam za mwenge

SERENGETI WAHITIMISHA MBIO ZA MWENGE KWA KUMWAGIWA SIFA
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akikabidhi risala ya Utii kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amour Hamad Amour katika Uwanja wa Mbuzi Mugumu ,kiongozi huyo amewamwagia sifa viongozi na wananchi kutokana na mpangilio mzuri wa mapokezi ya mbio za mwenge wilayani humo.
Amesema mbali na mipangilio mizuri pia miradi yao imetekelezwa kwa kiwango kinachowiana na gharama husika kutokana na ubora,pia jamii ya wakazi wa wilaya hiyo waishio nje ya wilaya wanavyochangia miradi ya kijamii ikiwemo ujenzi wa zahanati ya Busawe,Ofisi ya Kijiji na Bweni la wavulana Ngoreme sekondari.
Makamanda nao hawakuwa nyuma walikaa kwa umoja huku wakihakikisha ulinzi na usalama umeimarika
Brass band toka Tanapa walihanikiza katika mapokezi ya mbio za mwenge
Washiriki wakiwa katika makundi huku wakijjadiliana mambo kadha wa kadha
Makamanda wakiwa imara kabisa kusubiri maelekezo mengine
KLABU YA WAPINGA RUSHWA IKORONGO SEC SERENGETI YAKONGA NYOYO ZA WAKIMBIZA MWENGE KITAIFA
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour akikabidhi cheti cha ufunguzi wa klabu ya wapinga rushwa Ikorongo sekondari wilayani Serengeti baada ya kuridhishwa na uelewa wa klabu hiyo na kuagiza wafanye midahalo ndani na nje ya shule kuhusiana na athari za rushwa kwa jamii,kiuchumi na kiusalama,mwenge umemaliza mbio zake mkoa wa Mara na kuanza mkoa wa Arusha .
katika wilaya ya Serengeti jumla ya miradi saba imezinduliwa,kuwekwa jiwe la msingi na kufunguliwa ikiwa na thamani ya zaidi ya sh 1.9 bil.
Walinzi wa mwenge wakiwa kwenye majukumu yao
Katika maswali ya papo kwa na klabu ya wapinga rushwa Ikorongo sekondari ,kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa amekiri kuwa hakuna kama hao kwa uelewa hadi vifungu,na kuwamwagia sifa Takukuru kwa kuwaandaa vema vijana hao ambao watakuwa chachu ya mabadiliko kwa jamii kuepuka kutoa na kupokea rushwa ili kujenga taifa lenye maadili.
Kila aliyeguswa alijibu sawasawa licha ya kuwa na maswali ya mtego
Mambo yalivyokuwa Uwanja wa Mbuzi Mugumu
Meza ya klabu ya wapinga rushwa Ikorongo sekondari ikipitiwa na wakimbiza Mwenge kitaifa,hata hivyo mpangilio wao uliwakosha