Fahari ya Serengeti

Saturday, February 17, 2018

MATUMIZI YA VYOO BORA YATAPUNGUZA MAGONJWA YA KUAMBUKIZWA.

 Afisa afya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mugumu wilaya ya Serengeti Hellen Tupa akielezea athari za kutokutumia vyoo bora kwa wakazi wa kitongoji cha Kitahuru Kijiji cha Nyagasense ,baada ya kubainika kuwa wananchi wengi wanajisaidia vichakani.

Kupitia Mradi wa RAIN unaotekelezwa na amref health tanzania kwa kushirikiana na halmashauri kwa ufadhiliwa na Cocacola Africa Foundation ,amesema ujenzi wa vyoo bora na kuvitumia kutapunguza magonjwa ya kuambukizwa ambayo yanawagharimu fedha nyingi kwa ajili ya tiba.
 Wanafuatilia maelezo yanayotolewa.
 Usafi baada ya kutoka chooni ni muhimu kwa afya.





KARIBU SERENGETI WAZIRI

 Dc Serengeti Nurdin Babu kulia akimkaribisha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prjofesa Makame Mbawala baada ya kuwasili daraja la Kimkakati la Mto Mara kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa shughuli,daraja hilo lilianza kujengwa februari 2017 na linatarajiwa kukamilika aprili mwaka huu ,limegharimu zaidi ya sh 6.8 bil
 Salaam zinaendelea
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini akimkaribisha Waziri Mbawala
 Waziri Mbawala akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba

 Rc Kigoma Malima akijadili jambo na dc Nurdin Babu
Ukaguzi

RIGHT TO PLAY YAANDAA TIMU YA KUFUNDISHA KWA NJIA YA MICHEZO

 Mwezeshaji toka Right To Play Leah Tarimo akiongoza kipindi cha Changamoto za elimu  kwa kikosi maalum kinachounda na waratibu elimu na Wadhibiti Ubora wa Elimu wilaya yaSerengeti Mkoa wa Mara ambao watahusika na kuelimisha walimu ufundishaji kwa kutumi njia ya Michezo shuleni.
 Mmoja wa  washiriki akiwasilisha kazi za kikundi
 Washiriki wakiendelea na kipindi.
 Wanafuatilia mada


 Mratibu wa Shirika la Right To Play Serengeti Idd Ramadhani akiendelea na kazi wakati wa Mafunzo ambayo yameshirikisha Waratibu Elimu na Wadhibiti Ubora wa Elimu na Afisa Michezo wilaya.
 Sophia Chamuriho Mratibu elimu kata ya Mugumu akiwasilisha kazi ya vikundi
 Burudani za hapa na pale zilikuwepo
Uwasilishaji.

WAZIRI MBALAWA AWATAKA MAKANDARASI KUFANYA KAZI NZURI

 Meneja Tanroad Mkoa wa Mara Felix Ngaile akimwonyesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbawala eneo la daraja la Mto Mara linalotenganisha wilaya za Serengeti na Tarime linalojengwa na Kampuni za wazawa Gemen Engineering Company na Mayanga kwa zaidi ya sh 6.8 bil.
Amewataka kuhakikisha wanakamilika kazi hiyo mwezi aprili mwaka huu ikiwa ni pamoja na lami mita 90 kila upande.
 Ukaguzi una
 Waziri Mbawala akipata maelezo ya utekelezaji wa Mradi toka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Gemen Engineering Co. Mhandisi Andrew Nyantori jinsi wanavyotekeleza kazi hiyo.
 Anaeleza

Anasisitiza kuwa kazi itakamilika

Tuesday, February 13, 2018

KULA SAMAKI SASA NI ANASA NA BEI YA DAGAA YAPAA SERENGETI

 Bei ya dagaa katika mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara inazidi kupaa chanzo kikitajwa ni kudhibiti nyavu na makokoro yasiyokidhi hitaji la sheria,upatikanaji wake umekuwa wa shida katika soko la Mugumu hali ambayo inasababisha bei kupaa.
Kwa mjibu wa uchunguzi wa Serengeti Mesia Centre umebaini kuwa bei imepanda kwa asilimia 100 kwa kuwa kipimo cha sh 1000 sasa ni 2,000.

Aidha imebainika kuwa samaki wamekuwa adimu na wakipatikana bei yake iko juu ,ambapo wananchi wanadai kuwa kula samaki sasa ni anasa kwa kuwa samaki mdogo bei yake ni sawa na kilo moja ya nyama sh 5000.
 Baadhi ya wananchi wakinunua dagaa ambazo ndiyo mboga iliyotegemewa ya bei nafuu na wananchi wa wilaya hiyo.




WATU 14 WANASWA NA LITA 150 ZA GONGO NA MTAMBO WAKE

 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Juma Ndaki akionyesha mtambo wa gongo uliokamatwa katika kijiji cha Machochwe wilaya ya Serengeti ,katika operesheni hiyo katika kata za Nyansurura na Machochwe walikamata watu 14,lita 150 za gongo na mtambo mmoja wa gongo.
 Mtambo wa gongo
 Anaangalia mtambo wa gongo

MTUHUMIWA TOKA NCHI JILANI YA KENYA ANASWA NA AK AKIJIANDAA KUINGIA HIFADHI YA SENAPA


 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Juma Ndaki akiwa ameshukilia bunduki ya kivita aina ya AK 47 ambayo inadaiwa kukamatwa  na Polisi kwa kushirikiana na askari wa Senapa katika kijiji cha Machochwe wilaya ya Serengeti na risasi 27 zilizokuwa ndani ya Magazine,katika tukio hilo wamekamatwa watu wawili mmoja akiwa ni Raia wa Kenya na mwingine Tarime,inadaiwa walikuwa wanajiandaa kuingia ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili ya kufanya ujangili wa Tembo.



 Bunduki iliyokamatwa na risasi zake.



Baadhi ya askari Polisi wakiangalia Magazine na risasi zake.

Monday, February 12, 2018

GEITA SAMO PARALEGAL WAJENGEWA UWEZO MASUALA YA UONGOZI

Gervas Emmanuel Program Officer wa CWCA akitoa mada juu ya uongozi na usimamizi wa fedha kwa Paralegal wa Geitasamo wilaya ya Serengeti kwa ufadhili wa LSF.
Anasisitiza
Anakazia jambo
Paralegal wanafuatilia mafunzo