Fahari ya Serengeti

Tuesday, February 13, 2018

KULA SAMAKI SASA NI ANASA NA BEI YA DAGAA YAPAA SERENGETI

 Bei ya dagaa katika mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara inazidi kupaa chanzo kikitajwa ni kudhibiti nyavu na makokoro yasiyokidhi hitaji la sheria,upatikanaji wake umekuwa wa shida katika soko la Mugumu hali ambayo inasababisha bei kupaa.
Kwa mjibu wa uchunguzi wa Serengeti Mesia Centre umebaini kuwa bei imepanda kwa asilimia 100 kwa kuwa kipimo cha sh 1000 sasa ni 2,000.

Aidha imebainika kuwa samaki wamekuwa adimu na wakipatikana bei yake iko juu ,ambapo wananchi wanadai kuwa kula samaki sasa ni anasa kwa kuwa samaki mdogo bei yake ni sawa na kilo moja ya nyama sh 5000.
 Baadhi ya wananchi wakinunua dagaa ambazo ndiyo mboga iliyotegemewa ya bei nafuu na wananchi wa wilaya hiyo.




0 comments:

Post a Comment