Fahari ya Serengeti

Saturday, February 3, 2018

MIAKA 41 CCM VIONGOZI WAKEMEA WAAHIDI KUWASAKA WALIOHUJUMU MRADI WA MAJI RUNG'ABURE

 Dc Serengeti Nurdin Babu ameahidi kuchukua hatua kwa  wakazi wa kijiji cha Rung'abure watakaobainika walihusika kuhujumu mradi wa Maji kwa kukata mabomba na kusababisha wananchi zaidi ya 3200 kuendelea kuteseka kwa kununua  ndoo ya maji kwa sh 500 .

Katika maadhimisho ya miaka 41 ya CCM kiwilaya yaliyofanyika kijijini hapo,Babu amesema Mradi huo uliofadhiliwa na Benki ya Dunia ulilenga kutatua matatizo ya wakazi wa kijiji hicho,lakini baadhi ya watu kwa itikadi za kisiasa na wengine kujinufaisha kwa biashara ya kuuza maji walihujumu mradi huo huku serikali ya kijiji ikigoma kuupokea kwa madai kuwa haijakamilika.
 Baadhi ya wanachama wa CCM wakifuatilia hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali.

 Wanafuatilia
 Makundi mbalimbali ya wanachama yalikuwepo
 Nasisitiza
 Mimi ni kada wa CCM lazima jimbo lirudi mwaka 2020,amesema
 Katibu wa CCM wilaya Solomoni amesema kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wanachama wasaliti watadhibitiwa  ili kuhakikishawanakomboa jimbo na halmashauri.

0 comments:

Post a Comment