Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Nurdin Babu akielezea msimamo wa serikali dhidi ya watu wanaokaidi taratibu zilizopo wakati akitatua mgogoro kati ya meneja wa Shamba la Mathayo na eneo la Uhifadhi la Ikoma Culture Centre katika kijiji cha Bokore.
Amesema mifugo ya Mathayo ikikutwa katika eneo la uhifadhi wa asili atamkamata meneja wake Boniphace Chacha kwa kukaidi maagizo yake na kuvunja sheria zinazolinda maeneo hayo.
Kabla ya kutoa msimamo wa serikali wamepitia nyaraka mbalimbali na kubaini kuwa Ikoma Culture Centre ilipewa kihalali na serikali ya kijiji na hawatakiwi kuingiliwa .
Umakini wakati wa kutatua mgogoro umetumika kwa kupitia nyaraka moja baada ya nyingine na matumizi ya eneo,hivyo mifugo ni marufuku katika maeneo ya uhifadhi wa asili.
Hatimaye muafaka ukapatikana kuwa kila mtu aheshimu eneo la mwingine
Monday, February 26, 2018
Home »
» DC SERENGETI ATATUA MGOGORO WA WAFUGAJI NA UHIFADHI
0 comments:
Post a Comment