Fahari ya Serengeti

Saturday, August 5, 2017

ROBANDA WAKABIDHI NYUMBA YA POLISI YA ZAIDI YA SH 61 MIL


DC SSerengeti Nurdin Babu akimkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Jafari Mohamed nyumba ya askari Kituo kidogo cha Polisi Robanda iliyojenga na wananchi kwa zaidi ya sh 61 mil ikiwa ni mkakati wa kuimarisha ulinzi.
Nyumba hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia askari sita na itakuwa imemaliza tatizo la ukosefu wa nyumba kwa askari polisi walioko kituoni hapo.
 Ufunguzi ulifanywa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara

 Picha ya Pamoja ilipigwa baada ya kazi ya makabidhiano na kupongezana kwa kazi kubwa iliyofanyika

 Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Robanda Itabe Nkiri akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba hiyo iliyogharamiwa na kijiji hicho ili kuhakikisha wanaimarisha amani na usalama .

Rpc Mara akiongea na viongozi mbalimbali wa wilaya na kijiji cha Robanda 

Friday, August 4, 2017

UKOSEFU WA OFISI YA WALIMU SERENGETI SEKONDARI WAFANYIA KAZI CHINI YA MTI

Walimu wa shule ya sekondari Serengeti wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ofisi hali ambayo inawalazimu kufanyia kazi zao chini ya mti na wakati wa mvua hulazimika kukimbilia kwenye vyumba vya madarasa.
Oktoba mwaka jana bweni la wasichana katika shule hiyo liliungua na kusababisha watoto kukosa sehemu ya kulala na kuwalazimu walimu kupisha ofisi yao itumike kama bweni kwa ajili ya wanafunzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Juma Hamsini amesema kuwa wanamkakati wa ujenzi wa bwalo la chakula na ofisi ya walimu ili waweze kutoka katika mazingira hayo.
Shughuli zinaendelea kama kawaida

WASICHANA WAASWA KUZINGATIA MASOMO

 Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Molel akiwaasa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Serengeti  kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili waweze kufikia ndoto zao za maisha.

akikabidhi vitanda 15 na magodoro yake kwa ajili ya wanafunzi 30 wa bweni vyenye thamani ya zaidi ya sh 7.3 mil kwa ajili ya wanafunzi wa bweni amesema,misaada hiyo iwe chachu ya kufanya vizuri kwa kuwa jamii na wadau mbalimbali wanawatarajia waweze kusoma kwa makini wakiacha matendo ya ngono kwa kuwa athari yake ni kubwa.



SINGITA GRUMETI FUND YAIPIGA JEKI SHULE ILIYOUNGUA BWENI

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu kulia akipokea msaada wa vitanda 15 na magodoro yake kutoka kwa mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii ya Kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Molel yenye thamani ya sh 7,391,225 ambavyo vitasaidia watoto 30 waliokuwa wakilala chini kufuatia bweni la shule hiyo kuungua oktoba mwaka jana na kuteketeza vitu vingi ikiwemo vitanda.
 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akimshukuru Frida Molel kwa msaada huo ambao unapunguza ukubwa wa tatizo kwa watoto wa kike waliokuwa wanalala chini


 Baadhi ya vitanda vikifungwa
 wanakagua mazingira ya shule
wanafuatilia nyimbo kutoka kwa wanafunzi wa serengeti sekondari

Thursday, August 3, 2017

KUKOSEKANA KWA TAARIFA YA MWAKA KWASABABISHA BARAZA KUAHIRISHWA

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Porini katikati akijadiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Juma Hamsini kushoto na Mbunge wa jimbo hilo Marwa Ryoba baada ya kubainika kuwa kanuni za kikao cha madiwani zimekiukwa na wataalam kwa kushindwa kuwasilisha taarifa ya mwaka ambayo ingejadiliwa katika kikao hicho cha kawaida.

Katika kikao hicho madiwani walipaswa kuchagua makamu mwenyekiti,wenyeviti wa kamati,kuunda kamati na kupitisha ratiba ya vikao vya mwaka,kutokana na mapungufu hayo kikao kimeahirishwa huku wakiazimia kuchukua hatua kwa wataalam waliohusika kwa kuwa wanasababishia halmashauri hasara.
 Dc Nurdin Babu akijadiliana na Mwenyekiti wa halmashauri Juma Hamsini,Mbunge wa jimbo hilo Marwa Ryoba na Mkurugenzi Mtendaji Juma Hamsini ili kunusuru jahazi,hata hivyo kikao hicho kimeahirishwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Juma Hamsini akitoa maelezo ya kikao kabla ya kufunguliwa.
 Madiwani na wataalam wakifuatilia mjadala kikao kifanyike ama la,hata hivyo kimeahirishwa


 Diwani wa Mugumu Joseph Kihungwe(Mchina )ameacha dude na kusababisha kikao kuahirishwa baada ya kubainika kanuni zimekiukwa
 Madiwani n je ya kikao wakijadiliana
Mijadala kila kona iimefanyika baada ya kupata muda wa mapumziko ili mambo yawekwe sawa,hata hivyo uamzi wa mwisho kikao kimeahirishwa

Wednesday, August 2, 2017

MSTU WA AMANI MUHEZA TANGA KIVUTIO KIKUBWA CHA UTALII

 Wahariri wa habari na waandishi waandamizi wakipata maelezo ya Mstu wa asili wa Amani Muheza Mkoa wa Tanga muda mfupi baada ya kuwasili eneo hilo kwa ajili ya kuangalia vivutio vya utalii vilivyomo ikiwemo Mto Zigi na ufugaji wa Vipepeo.
 Timu ya waandishi ikisaka taarifa mbalimbali za mstu wa Amani

 Safari inaendelea
 Watoto wa kijiji cha Kisiwani kilichoko nje ya Mstu wa asili wa amani wakiangalia timu ya waandishi wakipita kuelekea mstu wa amani kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali za uhifadhi na utalii
 Taarifa zinatolewa.
 Mhifadhi wa Mstu wa Asili wa Amani Mwanaidi Kijazi akitoa taarifa mbalimbali za vivutio vilivyomo humo kwa timu ya waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali hapa Tanzania
 Kila mmoja anatafuta taarifa kwanini hiki kiko hivi ikiwa ni tofauti na maeneo mengine
 Jengo hilo lilitumiwa na wajermani kabla ya uhuru
 Wahenga wanasema mwenda pole hufika ,wanaendelea
 Kuelekea Mto Zigi unapita ndani ya mstu mnene

 Mambo yanaendelea
 Kilimo cha chai na uhifadhi wa mstu unafanywa na jamii ya hapo
 Mambo yanazidi kuongezeka
 Wahenga walisema ,mcheza kwao hutuzwa,wakazi wa Zigi na Kisiwani wakitoa burudani
Mijadala ya wao kwa wao ilichukua nafasi

VIJIJI VINAVYOUNDA JUMUIYA YA IKONA VYAPOKEA MAMILIONI YA FEDHA

 Viongozi wa Ikona Wma wilaya ya Serengeti wakiwa na viongozi wa vijiji wanachama wa jumuiya hiyo inayounda na vijiji vya Robanda,Parknyigoti,Nyichoka,Nattambiso na Makundusi wamepokea hundi ya zaidi ya sh 172 mil kwa kila kijiji ,ikiwa ni mgao wao wa fedha zilizotokana na mapato wanayokusanya,fedha hizo hutolewa asilimia 50 ya mapato yote kurudi kwa jamii ili kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
 Katibu wa Ikona Wma Yusuph Manyanda akitoa ufafanuzi wa mgao wa fedha kwa wajumbe,katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Elias Nchama na pembeni ni Makamu Mwenyekiti Jakobo Bega
 Wahenga wanasema penye jambo zuri kila mmoja hufurahi wanapiga makofi kuonyesha wanakubaliana na taarifa iliyotolewa.
 Viongozi wanafuatilia taarifa kwa makini
 Wengine wanakokotoa mahesabu na kuweka kumbukumbu sawa kwa kila hatua
 Mambo mazuri wanaonekana wakisema

 Picha ya Pamoja haikusahaulika

 Anachangia hoja
 Msisitizo ulitolewa na viongozi
Zote zimeenda vijijini