Fahari ya Serengeti

Thursday, November 30, 2017

WAZIRI AZINDUA UANDAAJI MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI WILAYA YA SERENGETI

 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea umuhimu wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi kwa vijiji .mji na Taifa wakati akizindua Uaandaji wa Mpango wa wa Matumizi Bora ya Ardhi wa wilaya ya Serengeti ambao unafadhiliwa na Serikali ya Ujermani kupitia Benki ya Maendeleo ya Watu wa Ujermani na Frankfurt Zoological Society(FZS) kwa zaidi ya sh 63 bil,kwa vijiji 40 wilaya za Serengeti na Ngorongoro,kati ya hizo sh 1.3 bil zitatumika kwa ajili ya Mpango bora wa Matumizi ya Ardhi na nyingine kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Kigoma Malima akielezea jinsi Mkoa ulivyojipanga kwa ajili ya kuhakikisha vijiji vingi vinapima ardhi kwa kutumia upimaji shirikishi.
Waziri anakabidi vifaa vya kazi kwa timu ya inayoshiriki zoezi hilo ambalo linafanywa na Frankfurt Zoological Society(FZS)Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Halmashauri ya wilaya ya Serengeti kwa ajili ya kuleta maendeleo na uhifadhi wa Ikolojia ya Serengeti.

Tuesday, November 28, 2017

KATIKA KUIMARISHA UWEZO MRADI WA RAIN WAWAJENGEA UWEZO WA MAFUNDI WA MAJI

 Katika kuhakikisha usimamizi imara wa Miradi ya Maji vijijini ,Mradi wa RAIN unaotekelezwa na amref helath africa na Halmashauri ya wilaya ya Serengeti kwa ufadhili wa COCACOLA  AFRICA FOUNDATION umewajengea uwezo wa kitaalam mafundi wanaotoka kamati za maji za Kata za Busawe,Kenyamonta,Mosongo na Nyansurura namna ya kufanya matengenezo panapotokea uharibifu,ikiwa ni njia ya kumilikisha mradi kwa jamii.
 Wananolewa.

9 WAFUNGWA KWA MAKOSA YA KUKUTWA NA NYARA ZA ZAIDI YA SH 107 MIL

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara imewahukumu kila mmoja miaka 20 washitakiwa 9  katika kesi nne tofauti baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Hakimu wa Mahakama hiyo Ismael Ngaile ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ni pamoja na vielelezo kama meno ya tembo,mafuta ya Simba,Mikia ya Nyumbu,na silaha za jadi Sime,pinde ,mishale na nyaya za kutegea wanyama.

Mwendesha mashitaka wa Jamhuri Emmanuel Zumba amesema makosa hayo yalitendeka kati ya mwaka 2016 na mwaka huu,na kuomba mahakama itoe adhabu kali kwa kuwa vitendo hivyo ni vya uhujumu uchumi.

SIKU 16 ZA KUPINGA UKEKETAJI WANAFUNZI SERENGETI WAFUNGUKA KUPINGA UKEKETAJI.

 Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Serengeti Maria Mchala akiwajengea uwezo wa kujitambua na kujisimamia katika maamzi  wanafunzi wa Kisangura sekondari ili kuepukana na vikwazo vinavyoweza kusababisha wasifikie ndoto zao kielimu kama mimba,ukeketaji na ndoa za utotoni.
Katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wilayani hapo,wadau mbalimbali na wanaharakati wamekutana na wanafunzi wa sekondari Kisangura kwa ajili ya kufikisha ujumbe unaolenga kuleta mageuzi makubwa ya kifkra.
Hata hivyo wanafunzi hao wamesema kuwa ukeketaji ni kikwazo kikubwa kielimu na wanatumia elimu yao kuelimisha jamii ili iweze kuachana na ukatili huo wa kijinsia.

 Wanafunzi wanafuatilia mjadala

 Afisa Vijana wilaya ya Serengeti akitoa mada.
 Meneja wa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti toka amref health africa Godfrey Matumu akibainisha ukubwa wa tatizo la ukeketaji kiafya na kisaikolojia.
Tunasikiliza

Wednesday, November 22, 2017

UTORO WAWASTUA WALIMUA







VIPANDE VYA NYAMA YA NYUMBU VYA MPELEKA GEREZANI MIAKA 20

MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA NYAMA KAVU ZA NYUMBU



Mwita Mwikwabe Chacha (42)mkazi wa kijiji cha Machochwe wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kukutwa na vipande 70 vya nyama kavu ya nyumbu vyenye thamani ya zaidi ya Tsh 56.8 milioni.

Katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 63/2016 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Ismael Ngaile ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo za kuhujumu mali za Umma.
Mapema Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri  Emmanuel Zumba mbele ya Hakimu Ismael Ngaile amesema kuwa ,aprili 15,2016 mshitakiwa alikamatwa nyumbani kwake Machochwe akiwa na nyara hizo kinyume cha Sheria.


ALAMBA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

MIAKA 20 JELA KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO

 Zakaria Wambura(52) Mkazi wa Kijiji cha Nyansurura wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara  amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kukutwa na meno mawili ya tembo yenye thamani ya Tsh 22.5 milioni.

Akitoa hukumu katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 106/2016,Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile amesema  mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka 20 kutokana na kosa hilo,ambalo ni kinyume na kifungu cha 86 cha Sheria Namba 5 ya Wanyamapori ya mwaka 2009.

Mapema Mwendesha mashitaka wa Jamhuri Emmanuel Zumba ameiambia Mahakama kuwa  mshitakiwa huyo alikamatwa oktoba 29,2016 ndani ya Pori la Akiba la Grumeti,akiwa na kisu,Shoka ,Panga na meno mawili ya Tembo kinyume cha Sheria.

Ameomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa kuwa wanyama hao wako hatarini kutoweka,huku mshitakiwa akiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa ni kosa lake la kwanza.

SERA YA ELIMU BILA MALIPO HAIJAELEWEKA



Wadau wa Elimu Ikoma Sekondari wilaya ya Serengeti wakiwa kwenye mjadala wa wazi ulioendeshwa na Marafiki wa Elimu wilayani humo ambao umeibua changamoto mbalimbali za elimu ikiwemo wazazi kutokuelewa maudhui ya sera ya Elimu msingi bila Malipo,na wamegoma kuchangia chakula cha watoto wakidai serikali inatoa.
Wanafunzi wa Ikoma sekondari wakifuatilia mjadala wa changamoto za elimu chini ya Marafiki wa Elimu.
 Mjadala unaendelea


 Rafiki wa Elimu Luzama Faustine akifafanua mada ya Mtoto na kuwataka walimu kutokutoa adhabu ambazo zinawafanya watoto wachukie shule

Wanafuatilia

Sunday, November 12, 2017

SANAA NURU WATIKISA MJI WA BUTIAMA KWA SANAA

 Kikundi cha Nuru Sanaa kutoka Mugumu Serengeti wametikisa mji wa Butiama kwa burudani mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Elimu uliofanywa na Twaweza -Uwezo mwaka 2015,miongoni mwa burudani zilizokonga nyoyo za wakazi wa mji huo ni ngoma ya Ritungu
 Timu Nuru Sanaa
 Wanafuatilia matukio mbalimbali kabla ya kuingia uwanjani kufanya yao
 Wanafunzi wa shule ya Butiama B wakiwasilisha ujumbe kwa igizo la Ukatili wa kijinsia kwa misingi ya milana desturi
 Nuru Sanaa wakifanya yao na kuwafnya wanafunzi kujitosa uwanjani kusakata ngoma ya Ritungu

Askofu wa kanisa la Anglican jimbo la Musoma Dk George Okothi akifafanua yaliyobainishwa na utafiti wa elimu katika wilaya ya Butiama









MGAO WA WALIMU UFANYIKE KWA UWIANO-ASKOFU

 Askofu wa Kanisa la Anglikan jimbo la Musoma Dk George Akoth ameitaka serikali kugawa walimu kwa uwiano ili kukabiliana na changamoto za watoto kutokujua kusoma na kuandika.

Askofu huyo ambaye ni Mratibu wa Mpango wa Taweza Uwezo Mkoa wa Mara amesema hayo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti waelimu katika wilaya ya Butiama iliofanyika mwaka 2015 ,amesema licha ya shule nyingi za vijijini kuwa na wanafunzi wengi zina walimu wachache na tatizo la kutokujua kusoma na kuandika ni kubwa kwa shule za vijijini ,suluhisho ni mgawanyo wa walimu uzingatie uwiano

Saturday, November 11, 2017

KILA SHULE BUTIAMA KULIMA EKARI MBILI ZA CHAKULA CHA WANAFUNZI

 Afisa Mtendaji wa Kata ya Butiama Hamisi Warioba Kwa niaba ya Dc wa Butiama Anarose Nyamubi akizindua ripoti ya utafiti wa elimu iliyofanywa na Twaweza kupitia Uwezo Mwaka 2015 wilaya ya Butiama na kubaini wanafunzi kutopata chakula ama uji kunachangia kuporomoka kwa taaluma.

Hata hivyo Warioba amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo kila shule inatakiwa kulimazaidi ya  ekari mbili za mazao ya mahindi ili kuwawezesha kupata chakula cha wanafunzi shuleni.
 Uzinduzi ukiendelea
 Kila kitu kiko hadharani ambapo imebainika wakati wa utafiti asilimia 25 ya walimu hawakuwa shuleni
 Utoro wa wanafunzi na walimu bado ni tatizo kubwa wilayani humo

 wanafuatilia

CHANGAMOTO ZA ELIMU ZAIBULIWA NA RIPOTI YA TWAWEZA BUTIAMA

 Akizindua Ripoti ya Utafiti ya mwaka 2015  iliyofanywa na Twaweza chini ya Mpango wa Uwezo Mratibu wa Mradi huo wilaya ya Butiama  Apaisaria Kiwori amesema,walibaini  asilimia 22 ya wanafunzi wa darasa la saba hawawezi  kusoma hadithi ya Kiswahili ya darasa la pili.

“Asilimia 38 ya wanafunzi wa darasa la saba hawawezi  kufanya hesabu za darasa la pili,huku asilimia 80 ya wanafunzi wa darasa la tatu hawawezi kufanya hesabu za darasa la pili,asilimia 9 ya wanafunzi wa darasa la tatu wanaweza kusoma hadithi za kiingereza ya darasa la pili,na asilimia 33 wanaweza kusoma hadithi ya Kiswahili ya darasa la pili,”alisema.
 Wanafunzi wa shule za msingi Butiama wakifuatilia taarifa ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti

 Wanaimba shairi

Wednesday, November 8, 2017

MARAFIKI WA ELIMU WAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI CHANGAMOTO ZA ELIMU

 Mratibu wa dawati la Jinsia la Polisi wilaya ya Serengeti Paul Pareso akielezea shughuli za dawati la polisi kwa upande wa ukatili wa kijinsia wakati wa mjadala uliowashirikisha wazazi,walezi walimu wa shule ya msingi Mugumu B,ulioandaliwa na Marafiki wa Elimu Serengeti
 Mratibu wa Marafiki wa ELIMU Serengeti Byabato akitoa ufafanuzi wa ushiriki wa Jamii katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kusomea kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Mugumu B,




 Ufafanuzi unatolewa